“If you have time to think before you start talking, think, Is it necessary to speak? Will what I have to say harm anyone?” – LEO TOLSTOY

Kabla hujaongea chochote, jiulize maswali haya mawili;
Je ni muhimu kuongea?
Je kile ninachokwenda kusema, hakitamdhuru yeyote?
Ukijiuliza maswali hayo na ukajipa majibu sahihi, mdomo wako hauwezi kukuponza.
Lakini pale unapoongea kabla hujafikiri na kujihoji maswali hayo, unajiingiza kwenye changamoto zisizo muhimu.

Ongea pale tu maneno yako ni bora kuliko ukimya,
Sema kilicho kweli na chenye msaada kwa wengine.
Kuongea ili tu na wewe uonekane una maoni, ndiyo chanzo cha kusema hovyo na kutengeneza changamoto mbalimbali.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kujihoji kabla ya kusema chochote ili kujiepusha na changamoto mbalimbali.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania