“We should get ready for death, because it will come, sooner or later. The best thing to do is to live a good life. If you live a good life, you should not be afraid of death.” – Leo Tolstoy
Kila mtu atakufa, hilo ni jambo ambalo halina ubishi.
Hivyo kuhofia kifo ni matumizi mabaya ya akili yako na muda wako.
Kitu sahihi kwako kufanya ni kuchagua kuishi maisha bora kwako,
Kwa sababu ukiyaishi maisha bora, huna sababu ya kuhofia kifo.
Kama kila siku utafanya kile ulichopanga kufanya, ambacho ndiyo muhimu zaidi,
Kama hutaahirisha chochote mpaka kesho,
Ukiimaliza siku unakuwa umeikamilisha,
Hivyo ukiipata siku nyingine inakuwa ni zawadi kwako.
Kuhofia kifo ni kiashiria kwamba hujayaishi maisha yako kwa ukamilifu.
Ukiyaishi maisha yako kwa ukamilifu, huna sababu ya kuhofia kifo.
Kifo kitakuja kwa wakati wake, wewe utakuwa bize na maisha yako.
Kuhofia kifo pia ni kiashiria kwamba haupo bize na maisha yako, huna makubwa unayofanya yanayokutaka ujisukume zaidi, hivyo unapata muda mwingi wa kufikiria na kuhofia vitu usivyoweza kudhibiti.
Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kuishi maisha yako kwa ukamilifu na kuacha kuhofia kifo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania