Men are born soft and supple;
dead, they are stiff and hard.
Plants are born tender and pliant;
dead, they are brittle and dry.
Thus whoever is stiff and inflexible
is a disciple of death.
Whoever is soft and yielding
is a disciple of life.
The hard and stiff will be broken.
The soft and supple will prevail.
– Lao Tzu.
Mtu anapozaliwa na anapokuwa hai, mwili wake unakuwa laini na unaobadilika (kukua).
Lakini mtu akifa, mwili wake unakuwa mgumu na usio na mabadiliko ya ukuaji.
Hivyo ulaini na kuwa tayari kubadilika katika ukuaji ni ishara ya maisha.
Ugumu na kutokubadilika ni ishara ya kifo.
Tafakari hili kwenye maisha yako, ni maeneo gani ya maisha yako umekuwa mgumu na hubadiliki?
Jua umechagua kufa kwenye maeneo hayo.
Kama unataka kuwa hai, lazima uwe tayari kubadilika, kwa kukua zaidi ya pale ulipo sasa.
Kila siku kazana kuwa bora kuliko siku iliyopita, ni ishara ya maisha na mafanikio.
Lakini kuendelea na mazoea, ni ishara ya kifo na kushindwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania