“Physical work, physical exercise for your body, is a necessary condition of life. A man can force others to do things for him, but he cannot free himself from the necessity of his own physical work. And if a man does not work at necessary and good things, then he will work at unnecessary and stupid things.” – Leo Tolstoy

Kazi inayohusisha mwili na nguvu ni muhimu sana kwetu sisi binadamu.
Tumeumbwa kwa namna ambayo tunaweza kufanya kazi.
Angalia mikono yetu binadamu, ni tofauti kabisa na ya viumbe wengine, imeumbwa maalumu kwa ajili ya kazi.

Hivyo kamwe usiache kufanya kazi,
Hata ukifikia uwezo wa kuwaajiri wengine wafanye kazi zako zote, usikubali kukaa bila kuwa na kitu cha kufanya.
Hata ukifikia hatua ya kutokuhitaji kufanya kazi tena, usikubali kuwa huna cha kufanya.

Kwa sababu unapokuwa huna kazi ya kufanya, unajikita muda na nguvu zako unavipeleka kwenye mambo ya hivyo, ambayo yanakuharibu zaidi.
Usipokuwa na kazi ya kufanya pia mwili nao unaona hauna matumizi, hivyo ubakaribisha magonjwa na hata kifo.

Tafuta kile ambacho unakipenda na kukijali kweli,
Kigeuze kuwa kazi yako,
Na ifanye kila siku ya maisha yako, mpaka siku unakufa.
Hakuna kustaafu wala kupumzika kwa siku nyingi.
Weka kazi, ina manufaa kwenye mwili, akili na roho.

Uwe na siku bora ya leo, siku ya kuweka kazi hasa, kwa sababu kazi unayofanya ndiyo utu wako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania