“If you love your enemies, you will have no enemies.” – Leo Tolstoy

Njia pekee ya kutokuwa na adui kwenue maisha yako ni kuwapenda maadui zako.
Kwa kuanza kabisa, mpende kila mtu na hutakuwa jata na adui wa kumpenda.
Kwa sababu unampenda kila mtu, hupati nafasi ya kumweka yeyote kwenye kundi la maadui.

Anayekupenda, mpende.
Anayekuchulia, mpende.
Anayekudharau, mpende.
Anayekukwamisha, mpende.
Anayekuibia, mpende.

Kila anayekuzunguka unapaswa kumpenda, kwa sababu anayakamilisha maisha yako.
Hata wale ambao unawaona ni waovu, wanaokuumiza na kukutesa, wapo kwenye maisha yako ili kuyakamilisha.
Huwezi kujua thamani ya upendo wa kweli kama hujawahi kuumizwa.
Huwezi kujua thamani ya kitu ulichonacho kama hujawahi kuibiwa.
Ukiwa na mtazano huu, ambao ndiyo sahihi, unajionea wazi kwa nini ni muhimu kumpenda kila mtu.

Swala anapaswa kumpenda sana simba,
Japo kwenye maombi ya swala anaweza kutamani simba wasiwepo kabisa,
Lakini pata picha kuna eneo lina swala pekee na hakuna simba.
Swala hao hawaliwi, wanazaliana kwa wingi na kupungua kwao ni kidogo.
Idadi yao inaongezeka, eneo la malisho lililopo haliwatoshi.
Majanga yanaanza kuwatokea, wanakosa chakula, magonjwa yanasambaa haraka kwa wingi wao na mwisho wanakufa kwa wingi.
Uwepo wa simba, unazuia jamii ya swala isifike kwenye majanga hayo, kwa kuwapunguza mapema.

Mpende kila mtu, haijalishi amekufanyia nini, jua kila mtu ni muhimu kwako.
Na ukimpa kila mtu nafasi ya umuhimu, hutakuwa na maadui wala kupoteza muda wako kwenye chuki.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kumpenda kila mtu na kufuta kabisa uadui unaoweza kuwa uliujenga huko nyuma.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania