Haijalishi umepiga hatua gani kwenye maisha yako, kuna mtu ambaye amepiga hatua zaidi kwenye eneo hilo.

Na uwepo wa watu ambao wamepiga hatua zaidi yako ni kiashiria kwamba hata wewe unaweza kupiga hatua zaidi ya hapo ulipo sasa.

Lakini je tunawezaje kupiga hatua kubwa kama ambazo wamepiga wengine?

Hili ni swali ambalo kila mmoja wetu huwa anajiuliza, lakini majibu ambayo wengi wetu tunajipa yamekuwa siyo sahihi.

Iko hivi, tukiona mtu amepiga hatua kwenye eneo fulani, huwa kwanza tunajiambia kwamba amepata bahati au upendeleo fulani, ambao sisi hatujaupata. Tunajiambia kwamba kama na sisi tungepata nafasi aliyoipata, basi tungefika hatua ambazo wamefikia.

Wakati mwingine tunaangalia ni kitu gani watu hao wamefanya na sisi kujaribu kufanya kama wao tukitegemea kufanikiwa kama wao. Lakini licha ya kufanya kile ambacho walipofanikiwa zaidi wamefanya, mara nyingi huwa hatupati matokeo kama yao.

Njia hizi mbili ambazo tumekuwa tunatumia sana hazitusaidii lolote, kwa sababu hazitupi majibu sahihi.

Njia sahihi ya kufikia viwango ambavyo wengine wamefikia ni kuwauliza swali muhimu, ambalo majibu yake yatatupa mwanga wa nini tufanye ili kufika walikofika wao.

Swali muhimu la kuwauliza waliokuzidi.

uliza vitabu anavyosoma.png

“If we encounter a man of rare intellect, we should ask him what books he reads.” – Ralph Waldo Emerson

Mwandishi na mwanafalsafa Ralph Waldo Emerson alitupa mwongozo sahihi wa kujifunza kutoka kwa wale waliotuzidi, iwe ni kiakili, kifedha au kimafanikio.

Emerson alisema iwapo utakutana na mtu ambaye amekuzidi, mwenye kitu ambacho wewe huna, unapaswa kumuuliza ni vitabu gani anasoma.

Hilo ndiyo swali unalopaswa kumuuliza yule aliyekuzidi rafiki, swali hilo ni; UNASOMA VITABU GANI?

Kwa nini swali hili?

Mtu yeyote ambaye amepiga hatua zaidi yako kwenye jambo lolote kuna vitu anajua ambavyo wewe hujui.

Kuna namna anafikiri na kufanya mambo yake, ambayo inamfikisha pale alipofika.

Wewe ukiiga kile anachofanya bila ya kuwa na namna ya kufikiri ambayo yeye anayo, hutaweza kufikia viwango alivyofikia.

Hivyo ukiuliza vitabu ambavyo mtu huyo anasoma au mambo anayojifunza, kisha na wewe ukajifunza, akili yako itafunguka na utaanza kuyaona mambo kwa namna tofauti na unavyoona sasa.

Ukishafunguka akili, unachukua hatua tofauti ambazo pia zinakupa matokeo tofauti na unayoyapata sasa.

Sina mtu wa kumuuliza.

Kama hapo ulipo hujakutana na wale waliofanikiwa sana ambao unaweza kuwauliza swali hili, wapo watu ambao wamesharahisisha swali hili.

Kuna mtandao unaitwa MOST RECOMMENDED BOOKS (www.mostrecommendedbooks.com) ambapo umekusanya mapendekezo ya vitabu kutoka kwa watu waliofanikiwa sana na kuvileta pamoja.

Hapa ni baadhi ya watu mashuhuri na waliofanikiwa na idadi ya vitabu ambavyo wameshauri watu wengine wavisome;

  1. Bill Gates (Bilionea, mwanzilishi wa Microsoft) – vitabu 206
  2. Jeff Bezos (Bilionea, mwanzilishi wa Amazon na tajiri namba moja duniani) – vitabu 13
  3. Elon Musk (Bilionea, mwanzilishi wa Paypal, Tesla na Space X) – vitabu 60
  4. Warren Buffett (Bilionea mwekezaji na mwanzilishi wa Berkshire Hathaway) – vitabu 46
  5. Mark Zuckerberg (Bilionea, mwanzilishi wa Facebook) – vitabu 39
  6. Steve Jobs (Aliyekuwa mwanzilishi wa Apple) – vitabu 15
  7. Charlie Munger (Bilionea, mshirika wa Warren Buffett) – vitabu 32
  8. Barack Obama (Rais mstaafu wa Marekani) – vitabu 31
  9. Oprah Winfrey (Bilionea, mtangazaji maarufu) – vitabu 83
  10. LeBron James (mchezaji mashuhuru)– vitabu 5
  11. Tim Ferriss (mwandishi na mwekezaji)– vitabu 108
  12. Richard Branson (Bilionea, mwanzilishi wa kampuni ya Virgin inayomiliki makampuni zaidi ya 400) – vitabu 66
  13. K. Rowling (Mwandishi wa vitabu vya Harry Potter) – vitabu 25
  14. Ryan Holiday (Mwandishi wa vitabu, mf. Obstacle is the way, Stillness is the key) – vitabu 57
  15. Ray Dalio (Bilionea mwekezaji) – vitabu 39
  16. Mark Cuban (Bilionea mjasiriamali na mwekezaji) – vitabu 12
  17. Malcolm Gladwell (Mwandishi wa vitabu, mf. Outliers, Blink, Tipping point ) – 31
  18. Seth Godin (Mtaalamu wa masoko na mwandishi wa vitabu, mf. Purple Cow, Linchpin, This is Marketing) – vitabu 27

Jinsi ya kupata vitabu vilivyoshauriwa na waliofanikiwa.

Rafiki, mpaka sasa umeshaelewa umuhimu wa kujua vitabu ambavyo waliofanikiwa sana wamevisoma. Pia umeshajua wapi pa kupata vitabu vilivyoshauriwa na wale waliofanikiwa sana.

Lakini huenda bado unakwama ni jinsi gani unaweza kupata na kusoma vitabu hivyo.

Hilo limerahisishwa sana kwako, kupitia programu ya SOMA VITABU TANZANIA, tunachambua vitabu hivi vilivyopendekezwa na wengi waliofanikiwa sana.

Kwa kujiunga na programu hii, unapata vitabu hivyo pamoja na uchambuzi wake kwa undani na hivyo kuondoka na mambo unayoweza kufanyia kazi na ukapiga hatua na kufanikiwa sana.

Karibu sasa ujiunge na programu hii ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; https://www.t.me/somavitabutanzania ukishafungua bonyeza JOIN CHANNEL na hapo utakuwa umejiunga na kuweza kupakua vitabu na chambuzi zake.

Hakuna kipya chini ya jua.

Ipo kauli kwamba hakuna kitu kipya chini ya jua, yote yanayotokea sasa yalishatokea tena huko nyuma, kwa sasa yanatokea kwa namna tofauti.

Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye mafanikio na utajiri, hakuna siri au njia mpya za kuelekea kwenye utajiri na mafanikio makubwa.

Njia sahihi ni zile zile, ambazo wengine walishazipita na kuziandika. Usitake kujaribu kupata njia hizo kwa kujaribu na kushindwa, badala yake jifunze kwa wale waliokutangulia kupitia usomaji wa vitabu.

Karibu kwenye channel ya SOMA VITABU TANZANIA (https://www.t.me/somavitabutanzania) ujifunze yale ambayo wengine walishayagundua na ufupishe safari yako ya mafanikio.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania