“If you see that some aspect of your society is bad, and you want to improve it, there is only one way to do so: you have to improve people. And in order to improve people, you begin with only one thing: you can become better yourself,” – Leo Tolstoy

Kama unaona kuna kitu hakipo sawa kwenye jamii yako au dunia na unataka kuibadili jamii au dunia, unaweza kufanya hivyo kwa kuwabadili watu.
Na njia pekee ya kuwabadili watu ni kwa kuanza kubadilika wewe mwenyewe.
Hivyo basi, njia pekee ya kuibadili dunia ni kuanza kubadilika wewe mwenyewe kwanza.
Kama hujawa tayari kubadilika, usitegemee dunia nayo ibadilike.

Kile ambacho unataka watu wafanye, anza kufanya wewe mwenyewe kwanza,
Ni rahisi kwa watu kufanya wakishakuona unafanya kuliko wakikusikia unawaambia cha kufanya.

Zoezi la kuibadili dunia kwa wengi ni gumu kwa sababu wao wenyewe hawapo tayari kubadilika.
Anza kubadilika wewe kwanza na kila kinachokuzunguka kitabadilika.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania