“All divine and human learning can be summarized in one truth—that we are members of one big body. Nature united us in one big family, and we should live our lives together, helping each other.” — LUCIUS ANNAEUS SENECA

Sisi binadamu wote ni kitu kimoja,
Kila mmoja ni kiungo muhimu cha mwili mmoja mkubwa ambao ni maisha.
Asili inatuleta pamoja kama familia moja kubwa,
Na njia pekee ya sisi kushinda kama binadamu, ni kushirikiana.
Katika ushirikiano kila mtu anakuwa na cha kutoa kwa wengine, na pia anakuwa na cha kupokea kutoka kwa wengine.

Tukiangalia historia yetu kama wanadamu, ni ushirikiano ndiyo uliotuwezesha kuwa viumbe wenye uwezo mkubwa zaidi duniani.
Viumbe wengine wote wanaishi kwa ubinafsi, kila mtu kupambana kivyake,
Lakini sisi binadamu tumeweza kuvuka hilo, mtu anaishi si kwa ajili yake tu, bali kwa ajili ya wengine.
Waliogundua moto, chuma, treni, umeme, magari, ndege, friji, tv, kompyuta, intaneti, simu janja na teknolojia nyingine nyingi, walikuwa hawajifikirii wao wenyewe tu.
Bali waliona mchango wao kwa maisha ya wengine pia, na kwa pamoja tumekuwa jamii bora.

Ukirudi kwenye historia pia, utaona mambo yalikuwa mabaya sana pale binadamu walipoanza ubinafsi.
Ukiangalia vita zote kubwa duniani, machafuko yaliyowahi kutokea na tawala za kidhalimu na kidikteta, vyote vilikuwa chimbuko la ubinafsi.
Ubinafsi wa mtu mmoja mmoja na ubinafsi wa jamii moja dhidi ya jamii nyingine umekuwa chanzo cha vita na machafuko yaliyowahi na yanayoendelea kutokea duniani.

Turudi kwenye asili na msingi wetu, tushirikiane, tuishi kwa ajili ya wengine.
Watendee wengine namna ambavyo wewe ungependa kutendewa.
Kama huwezi kusaidia, basi angalau usiumize wengine.
Wape wengine kile wanachotaka na utaweza kupata chochote unachotaka.

Uwe na siku bora sana ya leo, siku ya kushirikiana na wengine na kutoa thamani kubwa kwa ajili yao.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma

Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania