“A victory over oneself is a bigger and a better victory than a victory over thousands of people in a score of battles. Those who have achieved victory over other people can be defeated in future battles, but those who have achieved victory over themselves become victors forever.” —DHAMMAPAD
Ushindi wa kweli na udumuo ni ushindi dhidi yako mwenyewe.
Ukiweza kujishinda wewe mwenyewe ni bora kuliko kuwashinda maelfu ya watu.
Kwa sababu ushindi wako dhidi ya wengine ni rahisi kuangushwa,
Lakini ushindi dhidi yako mwenyewe hakuna anayeweza kuuangusha.
Ukijishinda wewe mwenyewe, unakuwa mshindi milele.
Ukiwashinda wengine, ni ushindi wa muda tu.
Shinda tamaa zako,
Shinda uvivu wako,
Shinda udhibiti wa fikra zako,
Shinda udhibiti wa muda wako.
Shinda kwenye nidhamu binafsi ya muda, fedha na kazi.
Jisimamie kwa uhakika.
Kwa kufanya hivyo utapata ushindi mkubwa na wa milele.
Jali mambo yako,
Wengine wamefanya nini haikuhusu,
Bali wewe umefanya nini ndiyo wajibu wako mkuu.
Ukijilinganisha na wengine umeshashindwa kabla hata hujaanza.
Ukijilinganisha na wewe mwenyewe hakuna wa kukushinda.
Huwezi kushinda kwenye mchezo ambao wengine wametunga sheria za mchezo huo.
Lakini mchezo wako mwenyewe, ambao umetunga sheria wewe,
Ushindi ni asububi kabisa.
Jishinde wewe mwenyewe na utakuwa ushindi mkubwa na udumuo.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania