“It is difficult to avoid working in life without either sinning, committing violence, being a party to violence, or by flattering and pleasing the agents of violence.” – LEO TOLSTOY
Chanzo kikuu cha maovu ni watu kukataa kazi.
Watu wanaiba kwa sababu hawataki kufanya kazi,
Wengine wanalaghai na kutapeli kwa sababu wanataka matokeo mazuri bila kazi.
Wapo pia wanaouza miili yao, na wengine utu wao ili kupata fedha bila kuweka kazi.
Wapo wanaokuwa na chuki na wivu kwa wengine, kwa sababu hawapo tayari kufanya kazi kama wao, na hao wengine wamewazidi kimafanikio.
Na wapo ambao wanakuwa omba omba kwa wengine kwa sababu tu hawapo tayari kuweka kazi.
Huwezi kuepuka na kukimbia kazi halafu ukabaki salama.
Lazima utaingia kwenye uovu fulani ili maisha yako yaweze kwenda,
Utafanya dhambi au kushiriki kwenye vurugu na ukatili au kukubaliana na wale wanaofanya hivyo.
Watu wengine wanaoingia kwenye kundi hili la kufanya maovu ni wale ambao wanafanya kazi wasizozipenda, kwa sababu wanataka tu kupata pesa.
Hapa watu hao hawafanyi kazi kwa moyo wao wote, wanatafuta njia mbalimbali za kuepuka kazi na wanakuwa wanasukuma tu siku ziende.
Japo wanapata pesa za kuendesha maisha, ndani ya nafsi zao wanakuwa wanapitia magumu sana.
Kinga na dawa ya uovu ni kufanya kazi,
Kuweka juhudi kubwa katika kutoa thamani kubwa kwa wengine,
Kuipa kazi kipaumbele kuliko vitu vingine,
Kupenda kazi unayoifanya na kuifanya kwa moyo mmoja.
Kuamini kwenye kazi na siyo kitu kingine chochote.
Penda kazi na weka kazi, na hutapata muda wa kuhangaika na maovu.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania