“The biggest happiness is when at the end of the year you feel better than at the beginning.” —HENRY DAVID THOREAU

Furaha iliyo kuu ni pale unapojiona ukiwa bora mwisho kuliko ulivyokuwa mwanzo.
Siku yako inakuwa ya furaha pale unapojiona uko bora zaidi mwisho wa siku kuliko ulivyokuwa mwanzo wa siku hiyo.
Kadhalika kwenye wiki, mwezi na mwaka.
Hili linatuonesha mambo mawili muhimu ya kufanya.

Moja ni furaha ni zao la ndani yetu, linalotokana na ubora wetu wenyewe.
Furaha siyo kujilinganisha na kuwashinda wengine,
Furaha siyo kupata kila unachotaka,
Bali furaha na vile unavyokuwa, ubora wako mwenyewe.

Mbili ni umuhimu wa kufanya tathmini kwenye siku, wiki, mwezi, mwaka na maisha.
Ni muhimu kila unapomaliza kipindi fulani, kukaa chini na kujifanyia tathmini, ulivyokuwa wakati unaanza na ulivyo wakati unamaliza.
Kila mwisho wa siku fanya tathmini, kuangalia ulivyokuwa mwanzo wa siku na mwisho wa siku hiyo.
Kila mwisho wa wiki, mwezi na mwaka pia fanya tathmini.
Tathmini hiyo inakuonesha wapi unafanya vizuri na wapi hufanyi vizuri.
Na unapofanya vizuri na kupiga hatua ndani yako, unatengeneza furaha halisi na idumuyo.

Kazana kuwa bora zaidi kila siku, ili unapoimaliza siku uwe bora kuliko ulivyooanza.
Hata siku moja usijiambie kwamba umeshafika kileleni na huwezi kuwa bora zaidi ya hapo.
Ukifika hali kama hiyo, utaanza kuanguka na kuwa hovyo zaidi.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania