To repay evil with goodness is easier, wiser, and more natural than to repay evil with evil. – Leo Tolstoy

Repay evil with goodness. —The TALMUD

Conquer rage with humility, conquer evil with goodness, conquer greed with generosity, and conquer lies with truth. —DHAMMAPADA

Kulipa ubaya kwa wema, ndiyo kitu sahihi, kitu rahisi na cha asili kufanya.
Hivyo mara zote lipa ubaya kwa wema.
Inakuwa rahisi na sahihi kwa sababu inamaliza mlolongo mzima.
Iko hivi, mtu akikufanyia ubaya, na wewe ukamjibu ubaya, unakuwa umempa sababu ya kufanya ubaya zaidi, na wewe utalipa ubaya zaidi.
Unajikuta mpo kwenye vita kubwa, kwa jambo ambalo lilikuwa dogo sana, mpaka unajishangaa mmefikaje hapo.
Lakini mtu akikufanyia ubaya, wewe ukajibu kwa wema, unakuwa umekata mzizi wa fitna, hawezi kupata ujasiri wa kufanya tena ubaya zaidi, labda kama atakuwa mwendawazimu.
Mtu yeyote mwenye akili timamu, atashangazwa na kuumizwa na wema uliomtendea baada ya yeye kukutendea ubaya na hatothubutu kuendeles na ubaya.

Kwa kifupi, chochote kisicho sahihi ambacho watu wanakufanyia, usiwajibu kwa kisicho sahihi, maana utakuwa umekihalalisha na kuwapa sababu ya kuendelea na kitu hicho.
Chukua mfano mtu amekutukana, ukimjibu kwa tusi unampa sababu ya kuendelea kukutukana, unakuwa umejishusha kwenye viwango vyake na hapo atakunyoosha.
Lakini ukimjibu matusi yake kwa maneno mazuri, atajikuta anaona aibu yeye mwenyewe, unakuwa umejiinua juu zaidi yake, na hapo utakuwa umemmaliza.

Njia pekee ya kushinda hasira ni unyenyekevu,
Kushinda ubaya ni kutenda wema,
Kushinda tamaa ni kuwa mkarimu,
Kushinda uongo ni kuwa mkweli.

Ukitaka kuzima moto kwa moto unaweza kufanikiwa, lakini kwa gharama na madhara makubwa sana.
Lakini kuzima moto kwa maji, yanayitumika kwa usahihi, ni rahisi, haraka na salama.
Lipa kinyume na ulichofanyiwa ambacho siyo sahihi na utakuwa umekikomesha kabisa.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania