Rafiki yangu mpendwa,
Kitendo cha wewe kuwa hai leo na kuweza kusoma hapa, ni jambo kubwa na la kushukuru sana.
Hicho ni kiashiria kwamba umeshinda vikwazo cha changamoto mbalimbali kwenye maisha yako.
Tangu kuzaliwa kwako mpaka hapo ulipofika sasa, umevuka mengi ambayo yamewapoteza kabisa wengi.
Hivyo haijalishi unajionaje au kujichukuliaje, wewe ni mshindi, umezaliwa kushinda na ndani yako umewekewa uwezo mkubwa sana.
Lakini cha kushangaza, asilimia kubwa ya watu wamekuwa hawatumii uwezo huu mkubwa unaowekwa ndani yao ili kufikia ushindi mkubwa zaidi.
Wengi wamekuwa wanaishi maisha ya kawaida na hilo limekuwa linawazuia kufurahia maisha yao, kwa sababu wanajua ndani yao wana uwezo mkubwa, ila hawautumii.
Niliandika kitabu kinachoitwa MIMI NI MSHINDI; Ahadi Yangu Na Nafsi Yangu, ili kumsaidia kila mtu kuvuka vile vikwazo vya ushindi ambavyo vipo ndani yake.
Watu wengi wamekuwa wanafikiri kwamba adui wa ushindi wao ni watu wa nje, lakini nikuhakikishie, adui mkubwa ni wewe mwenyewe.
Kwenye kitabu cha MIMI NI MSHINDI, nimekushirikisha hatua 20 za kukuwezesha wewe kuishi maisha ya ushindi kila siku.
Hapa nakwenda kukushirikisha mambo kumi unayopenda kufanya kila siku, ambayo yanakuzua isifikie ushindi wako.
- Hujachagua kuwa mshindi.
Hatua ya kwanza kuchukua ili kufikia ushindi kwenye maisha yako, ni kuchagua ushindi unaotaka kwenye maisha yako. Upo usemi kwamba kama hujui unakokwenda, njia yoyote itakuwa sahihi kwako. Hivi ndivyo wengi wanaendesha maisha yao, hawajui wanataka nini, ila wako bize kweli kweli.
Chagua leo unataka ushindi wa aina gani kwenye maisha yako ili uweze kuchukua hatua sahihi za kukufikisha kwenye ushindi huo.
- Hujachukua jukumu la maisha yako.
Kama umewahi kulalamika au kumlalamikia mtu mwingine juu ya jambo lolote linalohusu maisha yako, basi jua unajizuia kushinda. Washindi wanachukua jukumu la maisha yao kwa asilimia 100. Chochote kinachotokea kwenye maisha yao, wanajua wa kwanza kulaumiwa na kulalamikiwa ni wao wenyewe. Kulalamika na kulaumu ni rahisi, lakini inakufanya ujione usiye na hatia na uwezo wa kupambana kwenye maisha yako.
Amua leo kushika hatamu ya maisha yako, chukua jukumu la maisha yako kwa asilimia 100 kwa kutokulalamika au kumlaumu yeyote.
- Huamini kwamba unaweza kushinda.
Unapokutana na changamoto kidogo, unakata tamaa na kuona safari ya mafanikio haiwezekani. Watu wanapokupinga na kukukosoa unawasikiliza na kuona wapo sahihi kuliko wewe. Na hilo limekuwa kikwazo kwako. Ushindi unataka ujiamini kupitiliza, uamini unaweza kufanya chochote unachopanga, licha ya ugumu au changamoto unazopitia. Na ukweli ni kwamba, ukiamini na kuamua, hakuna kinachoshindikana.
Jiamini kwamba unaweza kushinda, licha ya magumu na changamoto unazopitia, endelea kuweka juhudi na utafikia ushindi mkubwa.
- Huna malengo yanayopimika.
Dhana yako ya malengo ni potofu, kwa sababu unajiambia tu kwamba mwaka huu nitafanikiwa zaidi, nitaongeza kipato, nitaanzisha biashara na kadhalika. Kujiambia kauli kama hizo siyo malengo, bali ni matamanio. Malengo ni pale unapopanga nini unataka, kwa kiwango gani na kufikia lini. Kama umepanga kuanza biashara, unajiambia kabisa ni biashara ya aina gani na utakuwa umeianza kufikia tarehe gani. Kama huwezi kupima malengo, huwezi kuyafikia.
Weka malengo yanayopimika na kila siku jipime kwa malengo hayo, gawa malengo hayo kwenye hatua za kuchukua na kila siku chukua hatua hizo bila kuacha na utafika kwenye ushindi.
- Umekosa uaminifu.
Umekuwa unasikiliza kauli za wale walioshindwa, ambao wanaamini wale waliofanikiwa kuna namna wamefanya. Utawasikia masikini wakisema matajiri ni wezi na walaghai. Utawasikia wasioweka juhudi wakisema waliofanikiwa wana bahati. Wengine wanakuja kwako na njia za mkato za kufanikiwa, ambazo hazihitaji kazi yoyote. Wewe kwa kutokuijua misingi ya mafanikio, unaingia kwenye mitego hiyo, kinachotokea ni unajikuta unapoteza muda wako na hakuna hatua unazopiga.
Chagua kuwa mwaminifu, kufanya kile kilicho sahihi kulingana na misingi ya mafanikio na siyo kudanganyika au kufuata mkumbo. Njia zisizo sahihi zinaweza kukupa ushindi, lakini hautadumu.
- Huweki kazi.
Umesikiwa watu wanakuambia usifanye kazi kwa nguvu, bali fanya kwa akili, wana kiingereza chao wanakuambia Don’t work hard, work smart. Ni uongo, hakuna ushindi unaopatikana bila kuweka nguvu na akili, tena kwa viwango vya juu sana. Watu wengi ni mashabiki na wafuatiliaji wa michezo mbalimbali. Nitajie mchezaji mmoja unayemkubali sana, ambaye wakati wenzake wanaenda kwenye mazoezi ya nguvu, yeye anafanya mazoezi kwa akili? Hakuna. Halafu wewe unajidanganya kwamba unaweza kufikia ushindi kwa akili bila nguvu!
Amua kuweka kazi, kazi hasa na siyo ya kitoto. Fanya kazi kwa juhudi na maarifa, nenda hatua ya ziada, toa thamani kubwa na ushindi utakuwa wako.
- Huthamini muda wako.
Unauchukulia muda wako poa sana, unautawanya kama vile una chemchem ya muda isiyo kauka. Unapoteza muda wako wa thamani kwenye mambo yasiyo na mchango wowote kwenye ushindi wako, kwa sababu hujui hata thamani ya muda huo. Unahangaika na habari mbalimbali, umbeya, udaku, maisha ya wengine na mengine mengi. Halafu unakuja kulalamika kwamba huna muda wa kufanya zaidi yale uliyopanga kufanya.
Upe muda wako thamani, jua ni kiasi gani cha kipato unataka kupata, kisha kigawe kwa masaa na jua saa yako moja ina thamani ya shilingi ngapi. Hivyo unapopoteza muda, unajua kabisa ni kiasi gani cha pesa umepoteza.
- Unazisikiliza sana hofu zako.
Hakuna mtu asiyekuwa na hofu, ila wewe unazisikiliza sana hofu zako, hivyo huthubutu kufanya kitu chochote kipya na kikubwa, kwa sababu unahofia kushindwa. Wanaoshinda wanapata hofu kama zako, lakini wanajua dawa ya hofu ni kufanya. Kuwa na hofu ni kawaida, ila kuzisikiliza hofu zako na kuzifuata ni kuchagua kuukosa ushindi.
Amua leo kuchukua hatua kwenye yale unayohofia, kwa sababu ndiyo yamebeba mafanikio yako na dawa ya hofu ni kufanya unachohofia.
- Hujifunzi kila siku.
Unapata muda wakula mara tatu kwa siku, kufuatilia habari, kufuatilia maisha ya wengine na kulala, lakini unajiambia huna muda wa kusoma vitabu. Hapo ndipo unapoagana na ushindi wako. Kwa sababu hakuna mshindi ambaye hajifunzi kila siku. Moja ya mahitaji ya maisha ya ushindi ni kila siku kuwa bora kuliko siku iliyopita, na ubora pekee utaupata kupitia kujifunza kila siku na kufanyia kazi yale unayojifunza.
Chagua sasa kujifunza kila siku, haijalishi siku yako imebana kiasi gani, hakikisha unatenga muda wa kujifunza kupitia usomaji wa vitabu na mafunzo ya aina nyingine. Usikubali siku ipite hujajifunza kitu kipya.
- Badala ya kuzalisha matokeo, unazalisha sababu.
Kabla hata hujaanza kufanya kitu, tayari umeshatengeneza sababu za kujitetea utakaposhindwa kwenye kitu hicho. Hivyo badala ya kuweka nguvu zako kubwa kuzalisha matokeo ya ushindi unayotaka, unapeleka nguvu hizo kuzalisha sababu za kujitetea. Huwezi kuzalisha sababu na matokeo kwa pamoja, chagua kuzalisha sababu na kuachana na matokeo au kuzalisha matokeo na kuachana na sababu.
Kataa kuwa mtu wa sababu, kuwa mtu wa kujisukuma kwa kila namna kupata matokeo unayotaka, usiwe mtu wa kukimbilia sababu.
Rafiki yangu mpendwa, haya ni machache na kwa kifupi sana kuhusu maisha ya ushindi. Mengi zaidi utayapata kwenye kitabu cha MIMI NI MSHINDI, Ahadi yangu na nafsi yangu.
Kitabu hiki ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Bei ya kitabu hiki kwa kawaida ni tsh elfu 10 (10,000/=), lakini kama utakilipia leo, utakipata kwa bei ya zawadi ambayo ni tsh elfu 7 (7,000/=)
Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 7 (7,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha MIMI NI MSHINDI na utatumiwa kitabu hicho.
Umezaliwa kushinda, nenda kaishi ushindi wako leo na kila siku kwa kuwa na mwongozo sahihi unaopatikana kwenye kitabu cha MIMI NI MSHINDI.
Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.
Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.
Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.
Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;
- KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
- JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
- JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
- KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
- BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
- MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
- IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
- PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.
Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.
Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania