Cato the Elder advised that in rainy weather, farmers must “try to find something to do indoors. Clean up, rather than be idle. Remember that even though work stops, expenses run on nonetheless.”

Kwenye kila siku yako, ogopa sana kuwa na muda ambao huna cha kufanya.
Huu ndiyo muda ambao unautumia kutengeneza matatizo zaidi kwenye maisha yako.
Hakikisha siku nzima umeipangilia, kila saa kuna kitu umeweka cha kufanya.
Pia hakikisha una kitu mbadala cha kufanya pale kile ulichokuwa umepanga kufanya awali kimeshindikana.

Kama ulipanga kufanya kitu fulani nje, halafu mvua kubwa ikaanza kunyesha, usikae na kujiambia huna cha kufanya.
Badala yake angalia ni vitu gani unaweza kufanya ukiwa ndani,
Hata kama ni kufanya usafi.
Muhimu ni mwili wako na akili zako viende kwenye kitu chenye manufaa na siyo kuviacha vikae tupu.
Asili huwa haipendi utupu, popote pasipo na kitu, panajazwa.
Acha chumba bila ya kitu chochote, kifunge kabisa, lakini utakapokuja kukifungua utakuta vumbi kila mahali.
Acha shamba nila kulilima wala kupanda chochote na baada ya muda magugu yatakuwa yameota kila mahali.
Kuwa na muda ambao hujaupangilia utafanya nini, ukija kustuka unazurura mitandaoni na kubishana mambo ya kijinga.
Asili haipendi utupu, hivyo tumia hilo kujaza kila muda wako na kitu cha kufanya, hata kama ni kupumzika.

Kuwa na muda mwingi ambao hujupangia vitu vya kufanya ndiyo chanzo cha matatizo mengi.
Tafakari matatizo yoyote uliyowahi kukutana nayo kwenye maisha yako.
Ni machache sana uliyapata ukiwa unafanya kazi au vitu vingine muhimu.
Mengi uliyapata ukiwa huna chochote muhimu cha kufanya.
Usiruhusu hili litokee tena kwenye maisha yako,
Pangilia vizuri muda wako wote.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania