“Our most important actions are those consequences which we will not see.” – Leo Tolstoy
Hatua bora na muhimu sana kwako kuchukua ni zile ambazo matokeo yake hutayaona wala kunufaika nayo wewe binafsi.
Kwa asili, sisi binadamu ni wabinafsi, huwa tunafanya kile kinachotunufaisha sisi kwanza kabla ya kufanya vitu vingine.
Na hakuna ubaya wowote kwenye hili, kwa kuwa ndiyo limetuvusha kama jamii ya wanadamu.
Hivyo kufanya kile ambacho kinakunufaisha wewe mwenyewe siyo jambo la kishujaa, kila mtu anaweza kufanya hivyo.
Lakini pale unapofanya jambo ambalo halikunufaishi wewe moja kwa moja,
Jambo ambalo huenda matokeo yake hutayaona kabisa,
Hapo ndiyo unakuwa umefanya jambo la kishujaa.
Kwa sababu unachukua hatua ambazo wanaokuja kunufaika ni wengine kabisa.
Mara kwa mara fanya zoezi hili,
Chukua hatua ambazo hazitakunufaisha wewe kabisa, lakini siku zijazo zitakuwa na manufaa makubwa kwa wengine.
Na hiyo itakuwa njia bora kabisa ya jina lako kuishi milele hata baada ya wewe kuondoka duniani.
Zoezi hili lipo ndani ya uwezo wako,
Siyo lazima kila wakati uangalie unapata nini,
Bali pia angalia unatoa nini hata kama hakuna unachoweza kupokea,
Na hilo litaonesha ni kiasi gani unaweza kufanikiwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania