“Kama huna biashara unayoweza kuiendesha ukiwa nyumbani kwako kwa kutumia mtandao wa intaneti, una tatizo mahali.” – Grant Cardone.

“Kama una simu janja (smartphone) na kila siku unaweka vocha ili kuingia mtandaoni lakini hakuna anayekulipa kwa kutumia mtandao basi unafanya makosa makubwa.” – Dr. Makirita Amani.

Rafiki yangu mpendwa,

Mlipuko wa virusi vya Corona unaoendelea duniani kwa sasa, umeipindua kabisa dunia. Kila kitu ambacho tulikuwa tumekizoea kinabadilishwa sana na hali hii inayoendelea.

Na eneo linaloguswa sana ukiacha eneo la afya ni eneo la uchumi.

Ili kupambana na usambaaji wa virusi hivi, njia kuu ambayo imekuwa inasisitizwa ni ya kuepuka mikusanyiko na kukaa nyumbani pale ambapo hakuna umuhimu wa kutoka.

Hili limeathiri sana kazi na biashara za wengi.

Wengi wamezoea kutoka nyumbani na kwenda ofisini au maeneo yao ya biashara ndiyo waweze kufanya kazi au kuuza na kupata kipato cha kuendesha maisha yao.

Lakini kwa sasa, hilo limebadilika, hata kama wewe utatoka, wateja unaowategemea hutawapata maana wengi wanakwepa mikusanyiko na kukaa majumbani kwao.

Hivyo huu ni wakati wa kuangalia jinsi gani unaweza kuiboresha kazi au biashara yako ili iweze kuendana na hali hii na isidhurike na hali kama hizi zinapokuja siku za mbeleni.

Mimi kama rafiki yako, jukumu langu limekuwa kukupa wewe maarifa sahihi yanayokuwezesha kufanya maamuzi sahihi na kupiga hatua kwenye maisha yako.

Na kwa hali inayoendelea sasa, ni muhimu sana uwe na uwezo wa kuingiza kipato bila hata ya kutoka nje ya nyumba yako.

Unapaswa kuwa na biashara ambayo unaweza kuiendesha ukiwa nyumbani na kuingiza kipato bila hata ya kukutana na wateja wako.

Hizo ndiyo aina ya biashara ambazo kwa sasa zinaendelea wakati ambapo kila aina ya biashara inaathirika sana.

Je ni biashara gani unayoweza kuingiza kipato ukiwa nyumbani?

Jibu ni biashara yoyote ambayo unaweza kuifanya kwa njia ya mtandao wa intaneti.

Kwa biashara hii, unatoa bidhaa au huduma kupitia mtandao wa intaneti na kisha wateja wanakulipa kwa njia mbalimbali za malipo zilizopo, ambazo hazihitaji kukutana ana kwa ana.

Biashara nyingi ambazo watu wamezoea kuzifanya kwa njia ya kawaida, zinaweza kugeuzwa na kufanyika kwa njia ya mtandao na ukaondoa gharama nyingi unazoingia ukifanya kwa njia ya kawaida.

Na hata kama kazi au biashara unayofanya kwa sasa haiwezekani kufanyika kwa njia ya mtandao, muda mwingi ulionao sasa unakutosha kuanzisha biashara nyingine ambayo unaweza kuiendesha ukiwa nyumbani kwako na kuingiza kipato bila ya kukutana na wateja.

Nimeandika kitabu kinachoitwa JINSI YA KUTENGENEZA FEDHA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Hiki ni kitabu ambacho kinakuwa mwongozo sahihi kwako kuanzisha biashara ambayo unaweza kuifanyia nyumbani au popote unapochagua mwenyewe.

KIPATO KWA BLOG

Kwenye kitabu hiki unakwenda kujifunza yafuatayo;

 1. Jinsi ya kutengeneza blog yako mwenyewe, hapo kuna maelekezo ya hatua kwa hatua na kwa picha jinsi ya kufanya hivyo.
 2. Njia mbalimbali za kuingiza kipato mtandaoni kwa kutumia blog.
 3. Jinsi ya kuchagua njia sahihi kwako kuingiza kipato mtandaoni.
 4. Jinsi ya kukuza blog yako na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi.
 5. Jinsi ya kuwageuza wasomaji na watembeleaji wa blog yako kuwa wateja ambao wanakulipa.

Na mengine mengi ambayo yanakupa wewe maarifa sahihi na hatua za kuchukua ili uweze kuingiza kipato hata kama hutoki nje ya nyumba yako.

Huhitaji mtaji ili kuanza.

Uzuri ni kwamba, kuigiza kipato mtandaoni kwa kutumia blog huhitaji kuwa na mtaji wowote wa kuanzia, kama unaweza kusoma hapa, basi kifaa hicho hicho unachotumia kusoma ndiyo unaweza kukitumia kuendesha blog yao.

Kama unatumia kompyuta hiyo hiyo inakutosha kufanya biashara hii. Na hata kama unatumia simu pekee, inakutosha sana kuweza kufanya biashara hii.

Unachohitaji kuwa nacho ni kitu kinachoongeza thamani kwenye maisha ya wengine na utayari wa kutoa thamani hiyo halafu kuwa na njia bora ya kulipwa na baada ya hapo kuweka kazi hasa.

Kipate kitabu ili ujifunze yote hayo na uanze kunufaika mara moja.

Jinsi ya kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG.

Kitabu hiki ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Bei ya kitabu hiki kwa kawaida ni tsh elfu 10 (10,000/=), lakini kama utakilipia leo, utakipata kwa bei ya zawadi ambayo ni tsh elfu 7 (7,000/=)

Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 7 (7,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha KIPATO KWA BLOG na utatumiwa kitabu hicho.

Ni wakati wako sasa wa kupinga kauli ya Grant Cardone kwa kuwa na biashara unayoweza kuiendesha ukiwa nyumbani kwako kwa kutumia mtandao wa intaneti.

Pia ni wakati wa kutumia vizuri vocha unazonunua na kuweka bando kwenye simu yako, badala ya kutumia kufuatilia yasiyo na umuhimu kwako, tumia kujiingizia kipato mtandaoni.

Pata leo kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG na uanze safari hii ya kuingiza kipato ukiwa nyumbani kwako.

Home-Work-1

Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.

Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.

Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.

Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;

 1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
 2. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
 3. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
 4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
 5. BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
 6. MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
 7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
 8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.

Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.

Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania