“Ignorance in itself is neither shameful nor harmful. Nobody can know everything. But pretending that you know what you actually do not know is both shameful and harmful.” – Leo Tolstoy
Ujinga siyo aibu,
Kutokujua kila kitu siyo vibaya,
Bali kujifanya unajua kile ambacho hujui ni jambo baya na la aibu.
Kwa sababu utawapotosha wengi na pia utawachelewesha kujua kila kilicho sahihi.
Kama kitu hukijui usione aibu kusema hujui,
Hakuna anayeweza kujua kila kitu.
Pia unapokiri hujui, unajiweka kwenye nafasi nzuri ya kujifunza kutoka kwa wale wanaojua.
Hili ni muhimu sana kulitafakari zama hizi maana ujuaji umekuwa mwingi.
Kwa mtu kujua kugoogle basi anaamini anajua kila kitu.
Mtu anaweza kusikia kitu kwa mtu mara moja na akageuka kuwa mtaalamu wa kitu hicho, akibishana na watu ambao ni wajuzi wa kitu hicho kwa undani.
Hakuna kitu kisochokuwa na ukomo,
Hivyo pia waepuke sana wale ambao wanaonekana kujua kila kitu,
Wale ambao hawakosi jibu la kitu chochote,
Hawa ni watu hatari sana kuzungukwa nao, kwa sababu watakupoteza vibaya sana.
Usione aibu kusema sijui, kama kitu hukijui kweli.
Usijisikie vibaya kuomba kufundishwa au kuelimishwa kile ambacho hukijui.
Hakuna aliyekuja duniani akiwa anajua chochote,
Na hakuna anayeondoka akiwa anajua kila kitu.
Chagua ni eneo gani unataka na ujuzi mkubwa nalo, kisha weka juhudi kujifunza eneo hilo.
Unapoulizwa kuhusu maeneo mangine yasiyohusiana na hilo, usione aibu kisema hujui.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha,nitaendelea kuwa mkweli na kujifunza kila Mara.
LikeLike