Rafiki yangu mpendwa,

Kama wewe ni fundi wa kitu chochote kile, unaweka nguvu kubwa kwenye kutengeneza kile unachouza, iwe ni nguo, samani, vifaa mbalimbali au nyumba. Ukishakamilisha kutengeneza kitu hicho, unakiuza na kupata fedha. Lakini kulipwa kunakuwa kumeishia hapo, ukitaka kulipwa tena ni mpaka utengeneze kitu kingine.

Kadhalika kama umeajiriwa, unalipwa mshahara kama umeingia kazini na kufanya kazi kila siku. Siku utakayoacha kwenda kazini, ndiyo siku mshahara huo unasimama.

Pia kama upo kwenye biashara ndogo, uwepo wako ndiyo kila kitu. Ukiwepo biashara inakwenda vizuri, usipokuwepo unaifunga au hata ukiwaachia wengine, hawataweza kuiendesha vizuri kama wewe.

Kwa kuangalia hali hizi ambazo tumezoea kukutana nazo kila siku, ni rahisi kuamini kwamba hiyo ndiyo njia pekee ya kuingiza kipato, kwamba lazima ufanye kazi kila wakati ndiyo ulipwe.

Vipi leo nikikuonesha kwamba ipo njia ya wewe kufanya kazi mara moja tu, na baada ya hapo ukawa unalipwa milele kwa kazi hiyo moja uliyofanya?

Utasema haiwezekani?

Jibu ni inawezekana, na hata wewe unaweza kufanya hivyo na ukanufaika sana maisha yako yote.

lipwa milele.jpg

Fanya kazi mara moja, lipwa milele.

Mtandao wa intaneti umerahisisha sana mawasiliano na pia umekuwa na manufaa makubwa kwa wengi, ikiwepo kuwafikia watu wengi zaidi kwa chochote ambacho mtu anakuwa amechagua kufanya.

Mtandao huu pia unatupa fursa ya kufanya kazi mara moja na kulipwa milele.

Hiyo ikoje?

Iko hivi, kwa kuandaa maarifa yako kwenye mfumo wa kidijitali na kisha kuyauza mtandaoni.

Kama kuna taarifa au maarifa yoyote unayo ambayo yanaweza kuongeza thamani kwa wengine, unaweza kuyaweka kwenye mfumo wa kidijitali, kitu ambacho unakifanya mara moja na baada ya hapo utakuwa unayauza milele.

Mfumo wa kidijitali ninaozungumzia hapa ni maandishi (words), sauti (audio) na video. Unachofanya ni kuandika kitabu na kukitunza kwa nakala tete (softcopy) au kurekodi audio au video yenye taarifa na maarifa hayo, na baada ya hapo kazi yako inakuwa imekamilika.

Kinachofuata baada ya hapo ni kuuza bidhaa yako ya kidijitali milele, huhitaji kufanya tena kazi ya kuandaa, unachohitaji ni kuwafikia wenye uhitaji na kuwauzia. Hivyo ndivyo unavyoweza kufanya kazi mara moja na kulipwa milele.

Hivyo tukirudi kwa watu tulioanza nao kwenye makala hii, iwapo fundi anayetengeneza vitu mbalimbali, ataamua kukaa chini na kuweka ujuzi na uzoefu wake kwa namna ambayo anaweza kuwauzia wengine, ataweza kuuza kwa maisha yake yote.

Kadhalika kwa mtu aliyeajiriwa, kama ataamua kukaa chini na kushirikisha uzoefu wake kwenye kazi hiyo, akaandaa bidhaa ya kidijitali, ataweza kuiuza maisha yake yote, bila kufanya kitu kingine kwenye bidhaa hiyo.

Kitu kimoja muhimu unachohitaji.

Kila mmoja wetu anaweza kufanya kazi mara moja na kulipwa milele, kwa sababu kila mtu ana ujuzi, maarifa, taarifa na uzoefu ambao unaweza kuwa na manufaa kwa wengine.

Hivyo kama mtu huyo ataweza kuweka maarifa hayo kwenye bidhaa ya kidijitali, atawanufaisha wengi.

Swali ni je mtu akishatengeneza bidhaa hiyo anaiuzaje milele?

Na hapo ndipo unapata jibu la kitu kimoja muhimu ambacho kila anayetaka kulipwa milele anapaswa kuwa nacho.

Kitu hicho ni blogu.

Kwa sababu siku hizi watu wanapokuwa na uhitaji hatua ya kwanza ni kutafuta kwenye google, unahitaji kuwa na njia ambayo watu watakufikia mtandaoni. Hivyo kwa kuwa na blog, wale wanaotafuta maarifa unayotoa, wanakufikia kwa urahisi wanapotafuta suluhisho la matatizo yao, na hapo ndipo wanakutana na maarifa yako na kuweza kuyanunua.

Kutokana na umuhimu huu mkubwa wa blogu katika kuuza bidhaa za kidijitali, ni muhimu sana kila anayetaka kulipwa milele kuwa na blog.

Jinsi unavyoweza kuwa na blog yako mwenyewe na kuitumia vizuri.

Swali muhimu kabisa unaloweza kuwa unajiuliza ni unawezaje kuwa na blog na utawezaje kuitumia kuuza bidhaa zako za kidijitali?

Hapa ndipo mimi rafiki yako nakuja kwako na suluhisho sahihi kwako.

Nimekuandalia kitabu kinachoitwa JINSI YA KUTENGENEZA PESA KWENYE MTANDAO KWA KUTUMIA BLOG. Ni kitabu ambacho kipo kwa nakala tete, ambacho kinakupa mafunzo ya jinsi ya kutengeneza blog yako mwenyewe, jinsi ya kuikuza na kuwafikia wengi na jinsi ya kuingiza kipato kupitia blog hiyo.

Kitabu hiki ni mfano halisi wa kufanya kazi mara moja na kulipwa milele. Kwa sababu nimekiandika mara moja na naendelea kukiuza kwa wale wenye uhitaji wa kujua jinsi ya kutengeneza kipato mtandaoni kama wewe.

Hivyo karibu sana upate kitabu hiki, ili hapo ulipo sasa, uweze kutumia kile kilichopo ndani yako kuwanufaisha wengine na wewe kunufaika kwa kipato utakachoingiza.

Kwenye kitabu hiki unakwenda kujifunza yafuatayo;

  1. Jinsi ya kutengeneza blog yako mwenyewe, hapo kuna maelekezo ya hatua kwa hatua na kwa picha jinsi ya kufanya hivyo.
  2. Njia mbalimbali za kuingiza kipato mtandaoni kwa kutumia blog.
  3. Jinsi ya kuchagua njia sahihi kwako kuingiza kipato mtandaoni.
  4. Jinsi ya kukuza blog yako na kuweza kuwafikia watu wengi zaidi.
  5. Jinsi ya kuwageuza wasomaji na watembeleaji wa blog yako kuwa wateja ambao wanakulipa.

Na mengine mengi ambayo yanakupa wewe maarifa sahihi na hatua za kuchukua ili uweze kuingiza kipato hata kama hutoki nje ya nyumba yako.

Huhitaji mtaji ili kuanza.

Uzuri ni kwamba, kuigiza kipato mtandaoni kwa kutumia blog huhitaji kuwa na mtaji wowote wa kuanzia, kama unaweza kusoma hapa, basi kifaa hicho hicho unachotumia kusoma ndiyo unaweza kukitumia kuendesha blog yao.

Kama unatumia kompyuta hiyo hiyo inakutosha kufanya biashara hii. Na hata kama unatumia simu pekee, inakutosha sana kuweza kufanya biashara hii.

Unachohitaji kuwa nacho ni ujuzi, maarifa, taarifa na uzoefu ambao unaweza kuongeza thamani kwenye maisha ya wengine na utayari wa kutoa thamani hiyo halafu kuandaa bidhaa ya kidijitali, (kitabu, audio au video) na kuwafikia walengwa kupitia blog yako ambapo utaweza kuwauzia zaidi.

Kipate kitabu ili ujifunze yote hayo na uanze kunufaika mara moja.

Jinsi ya kupata kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG.

Kitabu hiki ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Bei ya kitabu hiki kwa kawaida ni tsh elfu 10 (10,000/=), lakini kama utakilipia leo, utakipata kwa bei ya zawadi ambayo ni tsh elfu 7 (7,000/=)

Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 7 (7,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha KIPATO KWA BLOG na utatumiwa kitabu hicho.

Pata leo kitabu cha JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG na uweze kufanya kazi mara moja na kulipwa milele kwa kazi hiyo moja.

Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.

Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.

Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.

Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
  2. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
  3. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
  6. MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
  7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
  8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.

Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.

Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania