“Mankind has never achieved greatness but through suffering.” — F. ROBERT DE LAMENNAIS

Mateso ni njia ya kuelekea kwenye ukuu.
Hakuna mtu yeyote amewahi kufikia ukuu kwenye maisha yake bila kupitia mateso.
Na kadiri mtu anavyotaka kupata makubwa kwenye maisha yake, ndivyo mateso yake yanakuwa makubwa zaidi.

Chuma huwa inapitishwa kwenye moto mkali ili kuondos uchafu uliopo ndani yake.
Na chuma hicho hupitishwa kwenye moto mkali zaidi pale kinapotaka kufanywa kuwa imara zaidi.
Kadhalika kwetu binadamu,
Tunapitia mateso kwenye kupiga hatua kwenye maisha yetu,
Soma hadithi ya yeyote aliyefanikiwa na utajionea wazi nyakati za mateso kwenye maisha yake,
Nyakati ambazo wengine walikata tamaa,
Lakini yeye aliendelea kupambana, maana hakuwa na namna nyingine.

Tambua hili,
Mateso yoyote unayokutana nayo kwenye maisha,
Hayaji kwa ajili ya kukuumiza,
Bali yanakuja kwa ajili ya kukukomaza.
Kwa sababu sisi binadamu huwa tunaridhika na kuzoea vitu haraka.
Bilanya kukomazwa na magumu fulani, mafanikio yoyote tunayopata yatatuponyoka kabisa.

Yapokee mateso na magumu yoyote unayopitia kama sehemu ya wewe kuweza kukua zaidi.
Kwa sababu unapoyavuka, unakuwa umezaliwa upya,
Hakuna chochote kinachokuwa na nguvu ya kukuzuia.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania