“You should live so that it is possible to create the kingdom of love on earth. You should live a life based not on violence but on love.” – Leo Tolstoy
Unapaswa kuishi kwa namna ambayo unatengeneza ufalme wa upendo hapa duniani.
Ishi maishs ya upendo na siyo chuki, hofu wala ukatili.
Maisha yanapokosa upendo, ndipo matatizo na changamoto zote zinapozaliwa.
Chuki, hofu na ukatili ni zao la kukosekana kwa upendo.
Anza kwa kujipenda wewe mwenyewe, usipojipenda, huwezi kumoenda yeyote wala chochote.
Kisha wapende wengine, ukianza na wa karibu kwako. Kama huwezi kuwapenda wale ulionao karibu, huwezi kuwapenda wa mbali.
Halafu penda kazi au biashara unayofanya, usipopenda unachofanya, hutakuwa na msukumo mkubwa wa kukifanya na hivyo hutaweza kufanikiwa.
Kwa sababu mafanikio ni matokeo ya kurudia kufanya kwa ubora kile unachofanya,
Hivyo kupenda unachofanya kutakusaidia sana kuweza kukifanya kwa ubora kwa muda mrefu.
Amri iliyo kuu ni upendo,
Dini ya kweli ni upendo,
Jenga ufalme wa upendo kwenye maisha yako na utakuwezesha kupata chochote unachotaka.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Asante sana kocha, nitaendelea kuweka juhudi kubwa sana kwa vitu hivi vikuu, nguvu na muda zaidi ni kijua upendo ndio kila kitu kwa kufanya vitu ninavyopenda kidogo kidogo unakamilisha kitu kikubwa.
LikeLike