“Every great thing is done in a quiet, humble, simple way; to plow the land, to build houses, to breed cattle, even to think—you cannot do such things when there are thunder and lightning around you. Great and true things are always simple and humble.” – Leo Tolstoy

Kazi zote bora huwa zinafanywa kwa ukimya, urahisi na unyenyekevu.
Ukishajiona unafanya chochote kwa kelele, ugumu na majigambo, jua hakiwezi kuwa kikubwa na bora.
Fikiria kulima shamba, kujenga nyumba, kuandiks, kuzalisha wanyama na hata kufikiria.
Huwezi kufanya vitu hivi kwa kelele, ugumu na majigambo na ukapata matokeo bora.
Ni lazima uwe mtulivu, mnyenyekevu na ufanye kwa urahisi.

Siku hizi imekuwa nadra sana watu kuweza kufanya kazi zilizo bora,
Kwa sababu utulivu haupo kabisa.
Watu wanahangaika na mambo mengi ambayo hayana mchango wowote kwenye maisha yao.

Mitandao ya kijamii pia imezidi kuharibu mambo,
Watu wanatumia muda mwingi kujitangaza na kujigamba mitandaoni badala ya kuweka kazi.
Wengine wanapoteza muda mwingi kufuatilia maisha ya wengine mitandaoni badala ya kuhangaika na mambo yao.

Ni wakati sahihi kwako kufanya kilicho bora na kuachana na visivyo na umuhimu.
Kila siku jua ni matokeo gani unayotaka kuzalisha au wapi unapotaka kufika.
Kisha tafuta utulivu na fanya kazi yako, kwa urahisi na unyenyekevu.
Mengine yote hayana umuhimu kwako kwa wakati huo.

Ukiona badala ya kufanya kazi unajigamba, jua huwezi kufanya kazi hiyo.
Ukiona kazi rahisi unaifanya kuwa ngumu, jua hujajitoa kweli kupata matokeo.
Ukiona kila unapopanga kufanya kazi unaruhusu kelele ma usumbufu, jua unatafuta sababu ya kutokufanya kazi.

Utulivu, urahisi na unyenyekevu, ndizo hali unazohitaji kuwa nazo ili kufanya kazi iliyo bora.
Kila siku jijengee hali hizo ili uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania