Seneca said. “Anger always outlasts hurt,” he advised. “Best to take the opposite course. Would anyone think it normal to return a kick to a mule or a bite to a dog?”
Je na wewe utamng’ata?
Mtu anapokufanyia kitu ambacho hujapendezwa nacho, unakasirika na kupanga kulipa kisasi.
Je kama umembeba mtoto na akakukojolea, je na wewe utamkojolea?
Kwa akili za kawaida tu, wala halitakufikirisha, kwa sababu unajua mtoto kukojoa ni jambo ambalo halina kizuizi kwake.
Sasa inakuwaje mtu anakutukana na wewe unamtukana?
Kwa sababu hakuna mtu anayeanza kujifunza kutukana, bali wengi tayari wana tabia ya matusi.
Hivyo wewe kujibu tusi kwa tusi, ni kuwa sawa na aliyeanza kukutukana.
Seneca anatuambia hasira huwa inakaa muda mrefu kuliko maumivu ambayo tumeyapata.
Hivyo tunapaswa kuwa makini sana kutokuruhusu mamno yatukasirishe.
Anashauri tufanye kinyume na yale ambayo watu wametufanyia na yakatuumiza au kutukasirisha.
Kwa kufanya hivi unamzuia mtu asiendelee na kila anachofanya,
Na pia inakupa heshima kubwa kutoka kwa wengine.
Haijalishi ni jambo gani limetokea, usiruhusu hasirs ikutawale, kwa sababu hiyo itapelekea ufanye mambo yasiyo sahihi.
Pia jizuie sana kulipa ubaya kwa ubaya, kwa sababu hilo linakushusha kwenda kwenye hadhi ha yule anayekufanyia ubaya, ambaye tayari yuko chini yako, maana hakuna aliye juu yako anayekuwa na nia ya kukuumiza.
Kamba ambavyo ni upumbavu kumng’ata mbwa aliyekung’ata, ni upumbavu pia kumtukana aliyekutukana au kumwumiza aliyekuumiza.
Fanya kinyume na yake anayokufanyia mtu ili kukuumiza,
Kwa njia hiyo itadhibiti hasira zako na kuepuka kufanya yake yatakayokuumiza zaidi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania