Rafiki yangu mpendwa,

Umekuwa unafanya kazi ya kutangaza baadhi ya bidhaa na huduma unazozipenda na kuzikubali lakini hakuna mtu ambaye amekuwa anakulipa. Umekuwa unawashawishi watu wako wa karibu wenye uhitaji kama uliokuwa nao wewe, watumie kile ambacho wewe unatumia. Na kwa kuwa wanakuamini, basi wanatumia, hivyo unakuwa umepeleka wateja kwenye biashara hiyo, lakini wenye biashara hawajui kama umewapelekea wateja.

Tuchukue mfano huu, umekuwa na uhitaji wa kupata mtandao wa uhakika kwa pale ulipo. Lakini kampuni nyingi za simu hazina uwezo wa kutoa mtandao wa uhakika kwa eneo ulipo. Hivyo unajaribu kutumia makampuni mbalimbali na unakuja kukutana na kampuni Z ambayo huduma zake kwa mtandao kwa eneo ulipo ni za uhakika. Unazitumia na zinakupa matokeo unayoyataka.

Ukiwa unaendelea kutumia na kunufaika anakuja rafiki yako ambaye analalamika kwamba hapati huduma nzuri za mtandao. Unamuuliza ni kampuni ipi anatumia anakujibu kampuni X. Je wewe kama rafiki mwema utamwambia nini? Bila shaka utamwambia achana na kampuni X, tumia kampuni Z, na utamweleza ushuhuda wako wa jinsi ulivyohangaika na kampuni nyingi mpaka kufika kwenye  Z ambayo ina huduma za uhakika.

Kwa kuwa rafiki yako anakuamini, mara moja anakwenda kujiunga na kampuni Z ili naye apate huduma nzuri za mtandao. Kampuni Z inapata mteja mpya, lakini haijui kama ni wewe umempeleka, yenyewe inafikiri matangazo yake ndiyo yanafanya kazi, hivyo inalipa zaidi matangazo. Huku wewe uliyewapelekea mteja ukiwa hupati chochote.

NETWORK MARKETING

Ipo namna ya tofauti.

Vipi kama ningekuambia kwamba kampuni Z inaweza kukulipa kwa kila mteja unayempeleka? Vipi kama nikikuambia kampuni hiyo itaendelea kukulipa maisha yako yote kadiri mteja anavyoendelea kuitumia?

Unaweza kusema haiwezekani, unaweza kusema ni utapeli na mengine mengi.

Lakini hayo yote siyo kweli.

Upo mfumo wa kibiashara ambao unawatambua wale wanaoleta wateja kwenye biashara hiyo.

Mfumo huo unaitwa NETWORK MARKETING au MULTILEVEL MARKETING au DIRECT SELLING.

Kwa mfumo huu wa biashara, unakuwa na tatizo au uhitaji fulani, kisha unatumia bidhaa au huduma, inakusaidia na kuona watu wako wa karibu ambao wana uhitaji pia na kuwashawishi wanunue. Wanapokubali kununua, kampuni inakulipa sehemu ya faida ambayo inapata kama kamisheni.

Huu ni mfumo wa biashara ambao ni wa tofauti kidogo na hivyo wengi hawajauzoea. Lakini ni mfumo bora na rahisi kwa yeyote anayetaka kuutumia na anayependa kuwashauri watu kutumia vitu bora.

Wengi hujiuliza makampuni hayo yanapata wapi fedha za kuwalipa wale wanaoleta wateja wapya, na jibu ni kwamba makampuni haya yameepuka milolongo mingi ya kibiashara ambayo inaongeza gharama. Mfano gharama za kutangaza kwenye njia za kawaida na gharama za wauzaji wa jumla, kampuni hizi huwa zinauza moja kwa moja kwa mtumiaji wa mwisho, hivyo sehemu kubwa ya faida inabaki kwenye kampuni na hivyo kuweza kukupa wewe sehemu ya faida hiyo pale unapopeleka mteja.

Changamoto za aina hii ya biashara.

Pamoja na uzuri na urahisi wa biashara hii, ina changamoto moja kubwa, imevamiwa na matapeli wengi. Wale ambao wanataka kupata fedha kwa njia za mkato, wamekuwa wanakuja na makampuni yasiyo sahihi, kuwashawishi watu wajiunge ili wapate faida, mwisho wa siku waliojiunga wanapoteza fedha zao.

Pia kwa biashara zilizo sahihi, wale wanaowashauri wengine wajiunge wamekuwa wanawapa matumaini ambayo ni hewa, kwamba ukileta idadi fulani ya watu basi unapata fedha kiasi fulani. Hivyo sivyo biashara hii inavyofanya kazi.

Kutokana na kuvamiwa na matapeli, huku wanaoifanya wakiwapa watu ahadi hewa, watu wengi wameamua kutokiamini kabisa biashara hii ya mtandao, kitu ambacho kinawagharimu sana.

Ijue biashara ya mtandao kwa kina na jinsi ya kunufaika nayo.

Rafiki, kwenye kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING) nimeichambia biashara hii ya mtandao kwa kina,

Kuanzia msingi mkuu wa biashara hii,

Kisha mifumo ya ulipwaji kwenye biashara hii,

Halafu kuna vigezo vya kuangalia ili kujua kama kampuni ni sahihi kwako,

Pia kuna jinsi ya kujua kampuni ya kitapeli na kuiepuka,

Na pia kuna namna ya kunufaika na mfumo huu wa uendeshaji biashara kwenye biashara zako za kawaida.

Pata kitabu hiki na ukisome, utapata uelewa mpana kuhusu biashara ya mtandao na biashara kwa ujumla. Na hata kama hufanyi au hutafanya biashara ya aina hiyo, unaweza kutumia msingi wake kwenye kuifanya biashara yako ya sasa.

Hebu fikiria kama ungeweza kuwatumia wateja ulionao sasa na wakaleta wateja wengi zaidi, si biashara yako itakua mara dufu?

Basi hakikisha unapata na kusoma kitabu hiki cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO.

Jinsi ya kupata kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING).

Kitabu hiki ni nakala tete (softcopy) na kinatumwa kwa email. Bei ya kitabu hiki kwa kawaida ni tsh elfu 5 (5,000/=), lakini kama utakilipia leo, utakipata kwa bei ya zawadi ambayo ni tsh elfu 3 (3,000/=)

Kupata kitabu hiki, tuma tsh elfu 3 (3,000/=) kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na maelezo umelipia kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO na utatumiwa kitabu hicho.

Pata leo kitabu cha IJUE BIASHARA YA MTANDAO uweze kujifunza njia za kulipwa kwa kutumia bidhaa unayoipenda, lakini pia kuwatumia wateja ulionao sasa kupata wateja zaidi kwenye biashara yako.

Zawadi ya vitabu nane vya mafanikio.

Rafiki, nikukumbushe pia kwamba zawadi ya vitabu nane nilivyotoa inaendelea na karibu itafika ukingoni.

Kwenye zawadi hii, unapata vitabu nane nilivyoandika, katika mfumo wa nakala tete kwa kulipa nusu ya bei pale unapochukua vitabu vyote.

Vitabu hivyo na bei zake za zawadi ni kama ifuatavyo;

  1. KWA NINI MPAKA SASA WEWE SIYO TAJIRI, bei ya zawadi elfu 3.
  2. JINSI YA KUTENGENEZA KIPATO MTANDAONI KWA KUTUMIA BLOG, bei ya zawadi elfu 7.
  3. JINSI YA KUNUFAIKA NA MABADILIKO YANAYOTOKEA, bei ya zawadi elfu 3.
  4. KURASA ZA MAISHA YA MAFANIKIO, bei ya zawadi elfu 7.
  5. BIASHARA NDANI YA AJIRA, TOLEO LA KWANZA, bei ya zawadi elfu 7.
  6. MIMI NI MSHINDI, AHADI YANGU NA NAFSI YANGU, bei ya zawadi elfu 7.
  7. IJUE BIASHARA YA MTANDAO (NETWORK MARKETING), bei ya zawadi elfu 3.
  8. PATA MASAA MAWILI YA ZIADA KILA SIKU, bei ya zawadi elfu 3.

Ukichukua vitabu vyote nane kwa pamoja, unalipa tsh elfu 30 badala ya elfu 40 kama utachukua kimoja kimoja kwa bei ya zawadi.

Karibu sana upate zawadi hii, tuma fedha kwenda namba 0755 953 887 au 0717 396 253 kisha tuma ujumbe wenye email yako na jina la kitabu au vitabu ulivyolipia kisha utatumiwa kwenye email yako.

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania