“A bad mood is often the reason for blaming others; but very often blaming others causes bad feelings in us: the more we blame others, the worse we feel.” – Leo Tolstoy
Kuna mambo mbalimbali huwa yanatokea kwenye maisha yetu, mambo ambayo hatukutegemea yatokee.
Mambo hayo yanapotokea, huwa tunajisikia vibaya, kwa nini yatokee kwetu.
Hivyo huwa tunatafuta watu wa kuwalaumu kwa hayo yaliyotokea.
Tukiamini kwa kuhamishia lawama kwa wengine, basi tutajisikis vizuri, tutaona sisi na waathirika tu na kama siyo hao wengine, mambo yetu yangekwenda vizuri.
Lakini ukishalaumu wengine, unajisikia vibaya zaidi kuliko hata ulivyojisikia kwa kupata matokeo usiyotarajia.
Unazidi kujiona huna nguvu yoyote kwenye maisha yako na ni mtu wa kuathiriwa na wengine.
Unajiona wa hovyo na usiyestahili kupata unachotaka.
Hivyo matokeo ya kuwalaumu wengine, ni wewe kuzidi kujisikia hovyo kuliko ulivyokuwa awali.
Pamoja na kujisikia huko hovyo, bado unakuwa kama mlevi, inabidi utafute wengine zaidi wa kulaumu, au mengine zaidi ya kulaumu.
Kitu ambacho kinakufanya uzidi kujisikia vibaya.
Dawa kamili ya hili ni kuacha mara moja kulaumu mtu yeyote kwa jambo lolote linalotokea kwenye maisha yako.
Kila linalotokea, jipe jukumu kwamba ni wewe uliyesababisha na ni jukumu lako kurekebisha.
Kwa kujipa jukumu hilo, unapata nguvu na kujiona unaweza kufanya zaidi.
Unayaona maisha yako ni jukumu lako na hakuna yeyote wa kuyajenga au kuyaharibu ila wewe.
Unakuwa na uelewa kwamba maishs yako hayategemei kile wengine wanataka.
Bali ni matokeo ya kile wewe unataka na hatua unazochukua.
Acha sasa kulaumu au kulalamikia wengine,
Inakufanya uzidi kuwa hovyo kuliko kilichotokea.
Miliki maisha yako, pokea matokeo yoyote unayopata na kisha fanya kwa ubora zaidi.
Kufanikiwa au kushindwa kwenye maisha yako ni matokeo yako wewe mwenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania