“When a person sets to work, even if it is the most unqualified, primitive, simple work, the human soul calms down. As soon as a person starts to work, all the demons leave him and cannot approach him. A man becomes a man.” —THOMAS CARLYLE
Ipo dawa moja ambayo inaweza kuondoa kila aina ya pepo kwenye maisha ya mtu.
Dawa hiyo ni kazi.
Pale mtu anapofanya kazi anayoipenda na kuijali, ambayo inachukua muda wake na akili yake yote, roho yake yote inakuwa kwenye kazi hiyo.
Na hivyo anakuwa hana nafasi kwa ajili ya pepo kukaa ndani yake.
Lakini mtu anapokuwa hana kazi ya kufanya, au anafanya kazi ambayo haijali sana, roho yake inakuea na nafasi kubwa tupu ambayo inaruhusu pepo wa kila aina kuingia.
Kumbuka usemi kwamba akili na nafsi iliyo tupu ndiyo karakana na uovu.
Kila anayefanya uovu, ni kwa sababu ana muda mwingi ambapo hana kitu muhimu cha kufanya.
Ulevi, chuki, wivu na mengineyo, ni matokeo ya kukosa vitu muhimu vya kufanya.
Hivi unafikiri ukiwa na kitu muhimu unachofanya, ambacho kinatawala akili yako katika kufikiria namna bora ya kukifanya, utapata muda wa kuanza kufuatilia maisha ya wengine? Au kulewa? Au kuchukia wengine?
Huwezi kupata muda huo, kwa sababu muda wako mwingi unakuwa kwenye kazi na muda ambao unakuwa haupo kwenye kazi, unakuwa umechoka hivyo kuhitaji kupumzika.
Asubuhi hii yatafakari maisha yako kwa kina,
Kama kila wakati umekuwa unajikuta kwenye hali ambazo siyo nzuri au huzipendi,
Basi jua sababu ni moja, hukawa na kazi za kufanya ambazo zinataka akilo yako yote na roho yako yote.
Kama kila wakati unajikuta ukifanya makosa, kugombana na wengine, kuchukia, wivu na mengineyo, sababu ipo wazi, akili na nafsi yako vina muda mwingi ambao upo tupu.
Jaza akili na nafsi yako kwa kazi muhimu kwako, kazi unayoipenda na kuijali na weka umakini wako wote kwenye kuifanya.
Na utashangaa siku zako zikienda vizuri bila ya changamoto zozote.
Kazi ni tiba ya mengi, itumie vizuri.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania