“The true man is revealed in difficult times. So when trouble comes, think of yourself as a wrestler whom God, like a trainer, has paired with a tough young buck. For what purpose? To turn you into Olympic-class material.” – Epictetus

Tabia halisi ya mtu huwa inaonekana wakati anapitia magumu na changamoto mbalimbali kwenye maisha yake.
Huu ndiyo wakati ambapo mtu hawezi kufanya maigizo.
Yale unayoona watu wanafanya wakati wa matatizo na changamoto, ndivyo walivyo, huo ndiyo uhalisia wao.

Tumia matatizo na changamoto unazopitia kama njia ya kukazana kuwa bora zaidi.
Chukulia changamoto zako kama njia ambayo Mungu au asili inapima ukomavu wako. Kutaka kujua kama unaweza kuyakabili mafanikio makubwa, ambayo pia huja na majukuku makubwa.

Tumekuwa tunaona watu wanaokutana na bahati fulani kwenye maisha yao na mambo kwenda vizuri.
Lakini pale mambo yanapobadilika, wanakuwa hawana msingi sahihi wa kusimamia, kwa kuwa hawajawahi kusimamia chochote.
Baharia imara anatengenezwa wakati wa dhoruba.
Wewe imara unatengenezwa wakati wa matatizo.
Hivyo unapokuwa unapigia magumu, matatizo au changamoto mbalimbali, yakaribishe ukijua yanakuja kukufanya uwe imara kuliko ulivyokuwa awali.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania