“Progress is not achieved by luck or accident,” Epictetus said, “but by working on yourself daily.”
Kupiga hatua kwenye maisha yako hakutokani na bahati wala ajali,
Bali ni matokeo ya kazi ambayo unaiweka.
Na kazi hiyo siyo ya siku moja halafu unaacha,
Bali kazi unayoweka kila siku.
Viungo muhimu hapo ni KAZI na KILA SIKU
Wewe binafsi ni kazi inayoendelea,
Hivyo kazana kuwa bora zaidi kila siku,
Kazi kubwa inapaswa kuanzia ndani yako,
Kujenga tabia bora, nidhamu na kujidhibiti mwenyewe.
Kwa kuwa hivyo ndiyo muhimh kuliko hata mafanikio yenyewe.
Tumeona wengi ambao wamekutana na mafanikio kama bahati au ajali.
Lakini wakayapoteza yote kwa sababu hawakuwa tayari kwa mafanikio hayo.
Usiruhusu hilo litokee kwako,
Isifike siku ukaona umeshafika kilele na huhitaji tena kuweka kazi.
Kumbuka viungo muhimu ni KAZI na KILA SIKU
Utakapokwenda kinyume na hayo mawili, utakuwa umechagua anguko kubwa wewe mwenyewe.
Kwa sababu hata ukikutana na bahati au ajali yenye manufaa kwako, manufaa hayo hayatadumu kwa muda mrefu.
Kazi ya maendeleo binafsi, haina ukomo, ni kitu cha wewe kufanya kila siku.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania