“It seems that it is impossible to live without discovering the purpose of your life. And the first thing which a person should do is to understand the meaning of life. But the majority of people who consider themselves to be educated are proud that they have reached such a great height that they cease to care about the meaning of existence.” – Leo Tolstoy

Huwezi kuishi maisha bora na ya mafanikio kama hujalijua kusudi la maisha yako.
Na kitu cha kwanza kabisa unachopaswa kufanya kwenye maisha ni kujua nini maana ya maisha yako.
Lakini cha kushangaza, walio wengi wanaendesha maisha yao bila kujua kusudi wala maana ya maisha yako. Japo kwa nje wanaweza kuonekana wamefanikiwa na kupiga hatua, ndani yao wanakuwa na utupu mkubwa.

Rafiki, wewe na wanyama wengine kama mbuzi mnafanana kwa sifa nyingi kama viumbe hai. Kuzaliwa, kukua, kufa, kula, kutoa uchafu n.k.
Kitu pekee kinachokutofautisha wewe na mbuzi, ni ule utashi ulio ndani yako, ambao unakupa wewe nafsi, iliyo tofauti kabisa na watu wengine.
Nafsi hii ina kusudi la kuwa hapa duniani, inajua maana ya maisha yako.

Lakini cha kushangaza umeitelekeza nafsi yako na kuchagua kuishi kama mbuzi.
Kwa kufanya kile ambacho wengine wengi wanafanya na kuachana na maana ya maisha yako. Badala yake unakazana kumridhisha kila mtu kwenye maisha yako.

Hilo ndiyo linapelekea maisha yako kuwa magumu,
Licha ya kupiga hatua na kuonekana umefanikiwa,
Lakini bado ndani yako kuna kitu unakosa,
Kuna uhuru mkubwa unaoukosa,
Unajihisi kuna kitu hakipo sawa.
Lakini kwa bahati mbaya sana huwezi kujua ni nini,
Kwa sababu kwa maisha yako yotem hujawahi kukaa chini na nafsi yako na kuisikiliza inataka nini.
Umekuwa mtu wa kusikiliza wengine wanataka nini, wanakuchukuliaje na wanasemaje.
Kila muda akili na mawazo yako yamevurugwa,
Ukitaka kuyatuliza unatumia njia ambazo zinayavuruga zaidi na kukupoteza zaidi,
Kama kutumia vilevi, kuzurura mitandaoni na mengine.

Imetosha sasa, haifai tena kuendesha maisha yako kama mbuzi.
Ni wakati wa kuitambua nafsi kuu iloyopo ndani yako na kuisikiliza nini inataka.
Kisha kuifuata nafsi hiyo.
Itakuwezesha kujua kusudi na maana ya maisha yako.
Na ukitimiza hivyo, utakuwa na maisha bora sana, bila ya kujali umefikia wapi ukijilinganisha na wengine.

#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania