“Kazi ndiye rafiki wa kweli, asiyemtupa yeyote anayemheshimu.” – Dr Makirita Amani.
👉🏼Kazi ndiye rafiki wa kweli, imewatoa watu chini na kuwafikisha juu kabisa.
👉🏼Kazi inakupa heshima na utu, utaheshimika zaidi pale unapofanya kazi bora.
👉🏼Unapofanya kazi unayoipenda, inaacha kuwa kazi na kugeuka kuwa mchezo au sehemu ya maisha.
👉🏼Hakuna mbadala wa kazi, mtu akikuambia kuna njia ya kufanikiwa bila kazi, kimbia haraka, anataka kukutapeli.
👉🏼Onesha kazi unayoweza kuifanya kwanza kabla hujasema unataka kulipwa kiasi gani.
👉🏼Siyo kila mtu ataielewa kazi yako, hivyo fanya kazi na wale wachache wanaoielewa na kuithamini kazi yako.
👉🏼Kabla hujaianza siku yako ya kazi, weka vipaumbele vyako vizuri, anza kufanya yale magumu na muhimu.
👉🏼Tumia sheria ya 80/20 kwenye kazi, katika mambo 10 unayofanya, 2 ni muhimu zaidi kuliko 8 yanayobaki. Jua hayo mawili na weka juhudi zako zote.
👉🏼Tumia sheria ya Parkinson kwenye kazi, jiwekee muda wa ukomo ili kujisukuma kumaliza kazi kwa wakati.
👉🏼Fanya kazi yako, na waache wengine wafanye kazi zao. Kuna ambao watajipa kazi ya kukukosoa na kuwapinga, usihangaike nao, wewe endelea kufanya kazi yako, na waache waendelee na kazi yao.
👉🏼Kumbuka, unalipwa kwa thamani unayozalisha na siyo kwa masaa unayofanya kazi, kazana kuweka thamani zaidi.
👉🏼Penda sana kazi unayofanya, kazi inachukua karibu nusu ya maisha yako, kama hupendi unachofanya, unaharibu maisha yako kwa makusudi.
Heri ya siku ya wafanyakazi.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari bora,kwanza ya kufungua mwezi,pili ya Siku kuu ya wafanyakazi, hakika kwangu ni hotuba ya kutosha.
LikeLike