“The happiness or unhappiness of a man does not depend upon the amount of property or gold he owns. Happiness or misery is in one’s soul. A wise man feels at home in every country. The whole universe is the home of a noble soul.” —DEMOCRITUS
Furaha haitokani na mali ambazo mtu anazo,
Bali ni zao la rohoni.
Furaha au taabu huanzia ndani ya mtu mwenyewe na siyo nje.
Watu huanza kuwa na furaha kisha wanafanikiwa,
Na siyo kufanikiwa halafu ndiyo wakawa na furaha.
Watu huanza kuwa na taabu kisha wanashindwa,
Na siyo kushindwa halafu ndiyo wakawa na taabu.
Mtu mwenye hekima anaanza na kilicho sahihi rohoni mwake,
Hivyo anaweza kunufaika na kila hali anayopitia,
Anaweza kuishi kila eneo na kuishi na kila mtu.
Kwa sababu kilicho sahihi kinaanzia ndani yake,
Na hakitegemei wale wa nje wanafanyaje.
Usijiambie unasubiri ufanikiwe ndiyo uwe na furaha,
Bali anza na furaha na jiambie unataka kufanikiwa.
Hiyo ndiyo namna sahihi ya kuwa na maisha bora,
Kwa ubora kuanzia rohoni mwako.
Hakuna mafanikio yoyote utakayoweza kuyapata yakabadili roho yako.
Chochote ulichonacho sasa rohoni mwako, ukifanikiwa kitakuwa mara dufu.
Kama unajiona huna thamani, ukibahatika kufanikiwa ndiyo utajiona huna thamani zaidi.
Kama una chuki za aina fulani, ukifanikiwa chuki hizo zinakuwa maradufu.
Mafanikio huwa hayambadili mtu, ila yanakuza zaidi kile ambacho tayari kipo ndani ya mtu.
Hivyo jukumu lako la kwanza, ni kuwa sahihi ndani ya roho yako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania