“The rivers and seas are the masters of the valleys across which they flow. This is because they are lower than the valleys. In the same way, a person who wants to be higher than other people should be lower than they; if he wants to guide people, he should be below them.” —LAO-TZU
Mito yote hupeleka maji yake kwenye maziwa au bahari,
Kwa sababu maziwa na bahari hizi viko chini zaidi kuliko miyo hiyo.
Hivyo maji yanatiririka kutoka juu kwenda chini.
Maziwa na bahari ni kubwa kuliko mito, kwa sababu viko chini kuliko mito.
Hii ni kanuni ya asili ambayo tunaweza kuitumia kwenye maeneo mengine mengi ya maisha yetu.
Kama unataka kuwa juu ya wengine, basi anza kwa kuwa chini yao.
Kama unataka ukuu, kubali kuwa chini ya wengine.
Watu huwa tayari kutoa vitu kwa wale walio chini yao, kuliko wale walio juu yao.
Kama ilivyo rahisi kwa mto kutiririsha maji kwenda baharini kuliko kuyapandisha kwenda kilimani.
Wengi tumekuwa hatuielewi kanuni hii ambayo ni ya asili kabisa, na hivyo imekuwa inatukwamisha.
Tunajikweza sana na hapo wengine wanatuadhibu kwa kutotupa kile ambacho tulitaka watupe.
Kama tu tukiwa tayari kujishusha, kila mtu atakuwa tayari kutupa kile ambacho tunataka atupe.
Katika nyakati hizi ambapo kila mtu anajikweza,
Jishushe na hilo litakunugaisha sana.
Watu watajisikia salama kuwa na wewe,
Na watakuwa tayari kukupa kile unachotaka wakupe.
Ni kanuni ya asili, inafanya kazi bila kushindwa mara zote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania