Things that can be done at any time are often done at no time.
Kitu kinachoweza kifanyika muda wowote, huwa hakipati muda wa kufanywa.
Kitu kinachoweza kifanywa na mtu yeyote, huwa hakipati mtu wa kukifanya.
Kitu kinachoweza kufanyika eneo lolote, huwa hakipati eneo la kufanyiwa.
Hivi ni vitu vitatu muhimu sana unavyopaswa kuzingatia kwenye mipango unayojiwekea.
Unapopanga kufanya kitu, lazima uweke kwa uhakika kabisa vitu hivyo vitatu;
Utakifanya saa ngapi,
Utakifanya na nani,
Na utakifanyia wapi.
Andika kabisa na hapo fuata kama ulivyopanga.
Kujiambia nitafanya muda wowote ni kuamua tu kujidanganya, ni bora kujiambia ukweli kwamba hutakuwa na muda wa kukifanya.
Kusema kitafanywa na yeyote ni kujidanganya tu, ukweli ni hakitafanywa na yeyote.
Na kusema kitafanyika popote, ni kuona aibu kuukabili ukweli kwamba hakuna kinapoweza kufanyika.
Nitafanya kitu A siku na muda B, na mtu C eneo D. Rahisi kama hivyo.
Ili unapoacha kufanya, ujue kabisa kwamba umechagua kuacha kufanya na siyo kujipa visingizio kwamba hukupata muda, mtu au eneo la kufanyia.
Kushindwa kupanga, ni kupanga kushindwa,
Hivyo usianze kujikwamisha kwenye vitu vidogo kama hivyo vya mipango.
Panga kwa uhakika na kisha fanya kile ulichopanga.
Usijifiche nyuma ya kutokuwa na mpango, ni kujidanganya mwenyewe.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Mtu pekee wa kumwamini ni wewe mwenyewe,hivyo kupanga na usitekeleze ni sawa unajidanganya wewe mwenyewe.lakini iwapo utaiishi Siku yako vizuri kwa mpangilio uliopanga mwenyewe na ukatekeleza mipango yako hakika mwisho wa siku utakuwa mshindi wa mambo yako mwenyewe.
LikeLike
Hakika
LikeLike