Kama ambavyo nimekuwa nashirikisha mara kwa mara, na kama ambavyo taarifa mpya zinaonesha, ugonjwa huu wa covid 19 utachukua muda kuondoka.
Na mategemeo ya kuondoka kwa ugonjwa huu ni pale dawa au chanjo itakapopatikana, kitu ambacho kinakadiriwa kuchukua siyo chini ya miezi 18.
Hivyo tunapaswa kujifunza kuendelea na maisha katika hali hii,
Jambo ambalo litakuwa siyo rahisi.

Lakini pia kwenye darasa tulilopata jumapili, nilishirikisha changamoto kubwa mbili za ugonjwa huu wa covid 19 ambazo ni AFYA na UCHUMI.
Kwa changamoto ya afya tunapaswa kuendelea kujikinga na kukinga wengine, na nafasi ya kushinda hili kwa mtu mmoja mmoja ni kubwa.
Ila changamoto kubwa ni ya uchumi, kwa sababu mambo mengi yamesimama na hata pale mambo yatakapoanza kwenda tena, itachukua muda sana kwa mambo kuwa mazuri.

Kwa kifupi hakuna kitakachorudi kama kawaida, yaani kilivyokuwa mwanzo, kutakuwa na kawaida mpya, ambayo tunapaswa kujifunza kuishi nayo.
Kuna baadhi ya biashara zitakufa kabisa,
Kuna nyingine zitakuwa kwenye mdororo kwa muda mrefu.

Watu wengi wanazidi kupata hofu na kukata tamaa,
Lakini sisi kama wanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, tunapaswa kuwa tofauti.
Huu ndiyo wakati wa kutumia yale ambayo tumekuwa tunajifunza, na kuwa imara licha ya yote yanayoendelea.

Nitakuwa nashirikisha mbinu mbalimbali za kupambana na kawaida hii mpya katika kipengele cha #TuvukePamoja
Hii ni kusaidia kila mmoja wetu kuweza kuendelea na mapambano bila ya kukata tamaa.
Karibuni sana tuendelee kuwa pamoja, tuendelee na safari hii ya mafanikio na kukata tamaa kuwe mwiko ya kila mmoja wetu.
Hakuna aliyetuahidi kwamba safari hii itakuwa rahisi, hivyo tupambane.
Na uimara wetu unapimwa kwa changamoto tunazopitia na kuzivuka,
Ni wakati sasa wa kuonesha uimara tulionao.
Niwatakie wote kila la kheri.
Kocha.