“If a person has problems, there can he only one root cause: lack of faith. The same is true within human societies as a whole.” – Leo Tolstoy
Mzizi mkuu wa matatizo kwenye maisha yetu ni kukosa imani.
Hii ni kuanzia kwa mtu mmoja mmoja mpaka jamii kwa ujumla.
Tunapokosa imani, tunatoa nafasi ya hofu kutawala,
Na hofu ikishatawala, hakuna unachoweza kufanya.
Matatizo mengi tunayopitia ni kwa sababu ya kukosa imani.
Kukosa imani kwa nguvu iliyo kuu kuliko sisi, nguvu inayoendesha ulimwengu.
Kukosa imani kwenye uwezo mkubwa ambao uko ndani ya kila mmoja wetu.
Kukosa imanj kwenye mchango wa wengine na nguvu inayotokana na kushirikiana.
Hakuna asiyepitia matatizo na changamoto,
Lakini kinachowatofautisha wanaoshinda matatizo hayo na wanaoshindwa nayo ni imani.
Simamia imani, amini chochote bila ya kutetereka na imani yako itakuwa silaha kwako katika kushinda chochote unachopitia.
Imani haihitaji kuwa sahihi au siyo sahihi,
Bali imani inachohitaji ni kutokutetereka, kutokuwa na mashaka juu ya kile unachoamini.
Unapochagua unachoamini, achana kabisa na chochote kitakachoyumbisha imani yako.
Cha msingi ni imani yako ikupe matumaini kwamba mambo yatakiwa mazuri bila ya kujali nini unapitia sasa.
Na pia imani hiyo ikupe msukumo wa kuchukua hatua sahihi ili kuweza kutoka pale ulipo sasa.
Maisha bila imani ni sawa na gari bila mafuta,
Imani bila matendo ni sawa na gari yenye mafuta lakini haiendeshwi,
Kwa namna yoyote ile, hunufaiki na gari mpaka pale unapoiendesha.
Hivyo pia ndivyo ilivyo kwenye maisha, hunufaiki nayo mpaka uwe na imani yenye matendo.
Chagua leo unachoamini,
Jikumbushe hicho unachoamini kila wakati,
Chukua hatua kwa imani hiyo,
Usiyumbishwe waka kutetereka.
Na hakuna kitakachokushinda kwenye maisha,
Kama juhudi zako zitashindwa, basi muda utakusaidia.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania
Asante Sana kocha kwa tafakari, hakika neno Imani limezungumzwa Sana katika Biblia na ni sehemu kubwa ya mafundisho kwa viongozi wa dini kwenda kwa Wana damu,tatizo ni ukaidi wa kutojifunza zaidi na zaidi, Mara nyingi watu wanataka kuvuna bila kupanda,pasipo kujijengea nidhamu na misingi iliyo imara, Hakika mafundisho yako kwangu ni muhimu sana taratibu sasa naanza kuwarudisha watoto wangu,tunasoma pamoja,tunafanya mazoezi pamoja na wanaona tunavyoweza kwenda katika mabadiliko sahihi pamoja.
LikeLike
Vizuri sana Beatus.
LikeLike