Katika kipindi hiki tunachopitia sasa cha kuyumba kwa uchumi kutokana na mlipuko wa covid 19, ni nafasi nzuri kwa kila mmoja wetu kutoa thamani zaidi ya alivyokuwa anatoa awali.
Kwa shughuli yoyote unayofanya, iwe unazalisha au kuuza bidhaa au huduma zozote zile, nenda hatua ya ziada kwa kutoa thamani zaidi.
Nguvu yoyote unayoweka kwenye kile unachofanya, itakulipa zaidi baadaye.

Huu ni wakati mzuri wa kutoa thamani zaidi kwa sababu;
👉🏼Una muda mwingi kwa kuwa wateja au shughuli za kufanya kwa sasa siyo nyingi.
👉🏼Wengine hawajisukumi katika kipindi hiki, wengi wanakata tamaa na kufanya kwa mazoea.
Hivyo kama wewe utajisukuma kidogo tu, na kuweka thamani zaidi, utanufaika sana.

Manufaa utakayoyapata kwa kutoa thamani zaidi ni;
👉🏼Kuridhika kwa kile ambacho umefanya, unapotoa thamani zaidi unajisikia vizuri.
👉🏼Kulipwa zaidi na kuvutia wateja au kazi zaidi.
👉🏼Kupata hamasa ya kuendelea kufanya zaidi.

Anza sasa kutoa thamani zaidi kwa kila unachofanya.
Kama upo kwenye biashara kwa kila mteja unayempata kazana kumhudumia vizuri zaidi.
Kama umeajiriwa kwa kila jukumu unalofanya lifanye kwa viwango vya juu zaidi.
Fanya hivi na utavuka kipindi hiki ukiwa bora zaidi.
Kocha.