“In order to be happy, you should love—love with self-sacrifice, love all and everything, and spread a network of love everywhere. No matter who gets into this net, catch them all and fill them with love.” – Leo Tolstoy
Wanafalsafa na watu wenye hekima ambao wamewahi kupita hapa duniani,
Wote wanakubaliana kwenye jambo moja,
Kwamba kila tunachofanya ni kwa ajili ya kutafuta furaha.
Hakuna mtu anayeianza siku yake kwa kujiambia anataka awe na siku ya hovyo.
Bali kila mtu anaianza siku yake akitaka awe na furaha.
Ila sasa, wengi wamekuwa wanatumia njia zisizo sahihi kutafuta furaha.
Wengi wanahangaika na vitu ambavyo vinaleta raha ya muda mfupi na baadaye kuwa karaha.
Ulevi, ngono, udaku, vyote hivi vinaleta raha ya muda mfupi, lakini havileti furaha idumuyo.
Furaha inayodumu inatokana na kitu kimoja; UPENDO.
Kama unataka kuwa na furaha, basi unapaswa kupenda.
Kupenda kwa kujitoa kweli, kupenda wote na kila kitu bila ya kubagua.
Unapaswa kutandaza wavu wa upendo, na kila atakayeingia kwenye wavu huo, wajaze upendo.
👉🏼Anza kwa kujipenda wewe mwenyewe, kujikubali na kujithamini. Usipojipenda mwenyewe huwezi kuwapenda wengine au chochote. Huwezi kutoa kitu ambacho huna.
👉🏼Kisha wapende wale wanaokuzunguka, popote ulipo na kila unayekutana naye, mpende. Hata anayekuchukia wewe mpende. Kwa kuwa na upendo kwa wote, itapunguza sana migogoro yako na wengine.
👉🏼Halafu penda kile unachofanya. Sehemu kubwa ya maisha yako itapotelea kwenye kazi au biashara unayofanya. Hivyo kama utakuwa hupendi kile unachofanya, itaharibu upendo wako binafsi na upendo wako kwa wengine. Hivyo fanya kile unachopenda au penda kile unachofanya.
Upendo ni tiba, upendo ni kinga,
Upendo ni jawabu, upendo ni suluhisho,
Upendo ndiyo lugha inayoeleweka na kila mtu.
Upendo unakupa nguvu ya kuendelea kupambana,
Upendo unakuzuia usikate tamaa.
Upendo ndiyo dini ya kweli.
Kuwa na upendo wa kweli na utakuwa na furaha mara zote.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania