Katika kipindi hiki tunachopitia changamoto kubwa, uwekezaji sahihi kwako kufanya ni kuwekeza ndani yako binafsi.
Changamoto kama hizi zinatuonesha ni wapi tuna udhaifu na mapungufu, zinatuonesha nini tumekuwa tunafanya kwa mazoea.
Hivyo ni wakati sahihi kwako kufanya uwekezaji wa kuwa bora zaidi kwenye yale maeneo ambayo una udhaifu na mapungufu.
Chagua eneo ambalo unataka kuwa bora zaidi kwenye kazi yako, biasahra yako au maisha yako,
Kisha kipindi hiki, wekeza kwenye kujifunza na kuwa bora zaidi kwenye eneo hilo.
Jifunze kupitia usomaji wa vitabu vitakavyokupa maarifa sahihi kwenye eneo ulilochagua kuwa bora.
Pia jifunze kupitia kozi mbalimbali zinazotolewa mtandaoni, ambazo zinakupa maarifa sahihi na hatua za kuchukua kwenye eneo ulilochagua.
Hakuna wakati mzuri wa kuwekeza ndani yako kama sasa.
Na hakuna wakati ambapo ni rahisi kufanya hivyo.
Usikubali kuendelea kubaki ulivyokuwa,
Usikubali mapungufu na madhaifu uliyoyaona katika kipindi hiki cha changamoto yaendelee kuwa kikwazo kwako.
Wekeza ndani yako na utaweza kuvuka kipindi hiki ukiwa bora na imara zaidi.
Kocha.