Katika changamoto kubwa ya kiuchumi tunayopitia ambayo imesababishwa na mlipuko wa vizuri vya Corona, biashara nyingi zinakufa na kazi zinapotea.
Wengi wanafunga biashara zao na hawatakuja kuzifungua tena,
Wengi pia wanapunguzwa kazi na hawatakuja kupata kazi hizo tena.
Ni hali ambayo inawashtua wengi, kwa kuwa hakuna aliyeitegemea, maana kila kitu kilikuwa kinaenda vizuri.
Biashara zote ambazo zinakufa kipindi hiki, na kazi zote ambazo zinapotea, zinafanana kwa jambo moja; ZINAWEZA KUFANYWA NA KILA MTU.
Biashara zinazokufa na kufungwa kipindi hiki ni zile ambazo kila mtu anaweza kufanya, na hakuna kinachomtofautisha yeyote anayefanya.
Kwa lugha nyingine, biashara A isipokuwepo, wateja wanaenda kwenye biashara B na hakuna wanachokosa.
Kadhalika kwenye kazi, wanaopunguzwa kazi ni wale ambao wanachofanya kwenye kazi hizo kila mtu anaweza kukifanya. Hivyo John akiondoka, Juma anatekeleza majukumu yake na hakuna kinachopelea.
Njia pekee ya kuvuka kipindi hiki salama ni kutafuta eneo ambalo utahodhi, yaani ku-monopoly.
Kwenye kazi au biashara unayofanya, hakikisha kuna kitu unafanya wewe, ambacho hakuna mwingine anayeweza kufanya.
Usipokuwepo wewe pengo lako linaonekana wazi.
Kwa kujenga hali ya aina hiyo, unajilinda kwa janga hili na hate mengine yanayokuja.
Kama janga hili limekukuta ukiwa huna eneo unalohodhi, sasa ni wakati wa kuchagua eneo hilo na kutengeneza utofauti na utawala wako.
Kwenye kazi au biashara unayofanya, chagua kitu ambacho kitakutofautisha wewe, na hakuna mwingine atakayeweza kukifanya.
Na hili ni rahisi kama utaacha kuangalia wengine wanafanya nini, na kusikiliza nini kipo ndani yako.
Weka nafsi yako kwenye chochote unachofanya,
Na kwa kuwa hakuna wa kufanana na wewe, pia hakuna atakayeweza kufanya kama wewe.
Chagua eneo lako la kuhodhi,
Kila siku pambana kuwa bora na tofauti kwenye eneo hilo,
Na kwa hakika tutavuka pamoja kwenye changamoto hii na hata nyingine nyingi zijazo.
Kocha.