Mafanikio makubwa ni matokeo ya uvumilivu, ung’ang’anizi na msimamo.
Unahitaji kuwa na uvumilivu mkubwa kwenye chochote unachofanya, kwa sababu mambo hayatakuja haraka.
Unahitaji kuwa king’ang’anizi hasa kwa sababu utakwama na kushindwa, lakini hupaswi kukata tamaa.
Na pia unapaswa kuwa na msimamo, kufanya kitu kimoja mpaka pale unapopata majibu kabla ya kwenda kwenye kitu kingine.
Lakini jinsi wengi wanavyoendesha maisha yao, hawana uvumilivu, wanataka matokeo makubwa na wanayataka kwa haraka. Hawana ung’ang’anizi, wakishindwa mara moja hawarudii tena. Na pia hawana msimamo, kila mara wanajaribu kitu kipya wanachokutana nacho kabla kile walichokuwa wanafanya hakijaleta majibu waliyokuwa wanataka.
Andika maneno hayo matatu leo, na endelea kujikumbusha kila siku, nitavumilia, nitang’ang’ana na nitakuwa na msimamo. Ukizingatia hayo matatu, mafanikio yako ni swala la muda tu.
Kila la Kheri Rafiki Yangu.
Rafiki na Kocha wako,
Dr. Makirita Amani,
Nitavumilalia,nitang’ang’ania na nitakuwa na msimamo kwenye biashara yangu.Sitakuwa tayari kucompromise viwango nitakavyoweka kwa lengo la kumridhisha mteja.
LikeLike
Safi sana Hafidhi,
Iandike kauli hii mahali utakapokuwa unapata nafasi ya kuisoma kila siku,
Itakupa nguvu sana.
LikeLike
Asante kocha nitakuwa mvumilivu , king’ang’anisi na msimamo
LikeLike