“We often refuse to participate in the innocent joys of life because we are too busy with something we feel we have to do. We should accept these moments, because the sweet and joyful game is sometimes more important and necessary than most other things. Very often the business which busy people claim to be doing is not important at all, and sometimes it would be better left undone.” – Leo Tolstoy

Huwa tunajidanganya sana kwenye maisha,
Tunahangaika na kila kitu isipokuwa kuishi,
Kila wakati tunayasukuma maisha mbele tukiamini tutaanza kuishi baada ya kukamilisha kitu fulani,
Kinachotokea ni kila wakati tunakuwa bize na kile tunachotaka kukamilisha,
Na hivyo tunaachwa na maisha.
Ukiwa shule unakuwa bize na masomo na hivyo unajiambia utaanza kuishi ukimaliza masomo na kuanza kazi au biashara.
Ukianza kazi au bishara unakuwa bize na kazi na majukumu ya maisha na hivyo unajiambia utaanza kuishi ukistaafu na kumaliza malezi ya watoto.
Ukishastaafu na kumaliza malezi ya watoto, uzee unakuwa umekuingia na changamoto nyingine za kiafya zinakuwa zimekuingia.
Unachokuja kustuka ni maisha yamekupita ukiwa hujui.

Maisha ni kile kinachotokea wakati wewe uko bize na mambo mengine.
Na hakuna siku kila kitu kitakuwa sawa kama utakavyo ndiyo uweze kuanza kuishi.
Hivyo unapaswa kuanza kuishi sasa, kuishi kwenye kila wakati.
Usisubiri kumaliza chochote ndiyo uanze kuishi,
Bali unapaswa kuanza kuishi sasa.
Mambo mengi yanayokuweka bize,
Hayana umuhimu wowote.
Na kuthibitisha hilo tafakari siku moja iliyopita, wiki moja iliyopita na mwezi mmoja uliopoita.
Katika vipindi hivyo, umekuwa bize kweli kweli,
Lakini je, leo ni kipi unachokumbuka cha maana ulifanya kwenye huo ubize?

Mara nyingi tumekuwa tunatumia bize kama sehemu ya kujificha.
Hatutaki kuukabili ukweli kuhusu maisha yetu, hivyo tunahakikisha tunajisumbua kwa kujiweka bize.
Na tunaweza kuwa bize kweli, lakini ambacho hatuoni ni jinsi maisha yanavyotupita.
Chagua leo kuyaishi maisha yako kila siku na kataa kuwa bize kwa mambo yasiyo na tija kwako.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania