Rafiki yangu mpendwa,

Inapokuja kwenye kuweka malengo na mipango, watu wengi wamekuwa wanajiangusha kwenye maeneo matatu;

Moja wanaweka malengo ambayo ni madogo sana, hivyo malengo hayo hayawasukumi kuwa watu wa tofauti. Dawa; weka malengo makubwa ambayo yanakutikisa wewe na wengine, mfano kuwa bilionea.

Pili wanajipa muda mfupi wa kuyafikia, hivyo wanatafuta njia za mkato ambazo huwa siyo sahihi. Dawa; jipe muda wa kutosha wa kufikia malengo, angalau miaka 10.

Tatu hawapo tayari kufanya vitu vya tofauti na walivyozoea au wanavyofanya wengine. Dawa; ili upate ambacho hujawahi kupata, lazima ufanye ambacho hujawahi kufanya.

Kwa vikwazo hivyo vitatu, watu wamekuwa wanajikuta miaka inaenda lakini hakuna mabadiliko makubwa yanayotokea kwenye maisha yao.

Hata wanapokuwa na mabadiliko, ni ya kawaida sana, ambayo kila mtu anayo, labda mtu atakuwa na gari, au nyumba au vingine vya aina hiyo, lakini hakuna kikubwa kitakachotokea kwenye maisha yake.

Rafiki, napenda nikuambie kitu kimoja, kuishi maisha yako kwa ukawaida ni kuchagua kuyapoteza maisha yako. Hii ni kwa sababu, ndani yako una uwezo mkubwa sana wa kutenda miujiza, unaweza kufanya makubwa kuliko unavyofikiri.

Lakini hujapata mtu wa kukuambia hilo wazi, wala wa kukuonesha kwa vitendo.

Lakini nikupongeze kwa kusoma hapa, unakwenda kujifunza kwamba unaweza kufanya makubwa na pia unapata mshirika wa kwenda naye pamoja katika kufanya hayo makubwa.

Muongo wa kuwa Bilionea.

Rafiki, kama umekuwa unanifuatilia kwa muda, unajua kabisa nimekuwa nakushirikisha malengo yangu makubwa mawili, ambayo ni kuwa bilionea mpaka kufikia mwaka 2030 na kuwa raisi wa Tanzania mwaka 2040.

Sasa mwaka huu 2020 ulipoanza, niliandika kwenye dayari yangu kwamba kati ya mwaka 2020 mpaka mwaka 2030 ndiyo muongo wa mimi kufikia lengo la kwanza, ambalo ni kuwa bilionea.

Hivyo nimejipa miaka hii kumi, ya kupambana kwa kila namna kuhakikisha lengo hilo ninalifikia kama nilivyopanga.

Na njia kuu ambazo ninazitumia kwa sasa ni uandishi, utabibu na uwekezaji. Kwenye makala ya kumbukizi ya kuzaliwa kwangu nimekushirikisha mpango wa kuandika vitabu 100 ndani ya miaka hiyo 10.

Hivyo lengo la awali ni kufikia dola bilioni 2 mwaka 2030, ambayo kwa wastani itakuwa kama tsh trilioni 5. Hii trilioni 5 ukigawa kwa vitabu 100, inabidi kila kitabu kiingize bilioni 50. Kama kila kitabu kitauzwa kwa wastani wa tsh elfu 5, basi kila kitabu kinapaswa kuuza nakala milioni 10.

Hivyo rafiki, milioni 10 ndiyo namba ninayoanza kuifanyia kazi.

Kwa sasa ninaandaa jukwaa ambalo litakuwa linabeba vitabu hivyo, na ili mtu aweze kuvisoma atapaswa kujiandikisha kisha kununua na kusoma. Hiyo ina maana nahitaji kufikia watu milioni 10 waliojiandikisha kwenye jukwaa hilo kufikia mwaka 2030.

Huo ndiyo mpango wa awali ambao naufanyia kazi, nitaendelea kuuboresha kadiri ninavyokwenda na kulingana na matokeo ninayopata. Lakini muhimu ni kwamba tayari ninayo namba ninayoifanyia kazi.

Lakini pia kuna vyanzo vingine vya kipato na uwekezaji unaoendelea na utakaokuwa unaendelea, hiyo sijaweka kwenye hesabu hizo, lakini yatasaidia lengo kufikika hata kama namba hazitaenda kama nilivyopiga hapo.

Karibu tusafiri pamoja.

Rafiki yangu mpendwa, je na wewe unapenda kufikia ubilionea kwenye kipindi hiki cha miaka 10? Je umeshachagua ni eneo gani unakwenda kuchuma mabilionea yako?

Kama jibu ni ndiyo basi karibu sana tusafiri pamoja. Kwa kusafiri pamoja tutashirikishana njia bora za kuhakikisha tunafikia malengo haya makubwa.

Ili tuweze kusafiri pamoja, unapaswa kuwa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, hivyo kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, chukua hatua ya kujiunga sasa. Na kama tayari umeshakuwa mwanachama, basi hakikisha hupotezi sifa ya uanachama kwa kutekeleza majukumu yako kama mwanachama.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania