Rafiki yangu mpendwa,

Wiki chache zilizopita nilipata nafasi ya kukaa chini na mwandaaji wa kipindi cha Kabati La Vitabu, Irene Kamugisha ambaye alikuwa na maswali mbalimbali kuhusu mambo niliyoandika kwenye kitabu cha ELIMU YA MSINGI YA FEDHA.

Maswali yalikuwa mazuri na nilipata nafasi ya kutoa ufafanuzi wa mafunzo mbalimbali yaliyopo kwenye kitabu na hatua muhimu za kuchukua.

Hapa nakushirikisha nafasi nzuri kwako kusikiliza kipindi hicho ambacho kimewekwa mtandaoni, hivyo unaweza kukisikiliza kwa muda wako.

Kusikiliza kipindi hicho, BONYEZA MAANDISHI HAYA au fungua kiungo hiki kusikiliza; https://wp.me/p4VYpK-79q

Rafiki, nikuambie tu hiki ni kipindi bora sana kwako kusikiliza ambacho kitakusaidia sana kwenye eneo la fedha, tenga muda na ukisikilize.

Kwenye kipindi hiki, utapata ufafanuzi wa kina wa mambo yafuatayo;

1. Umuhimu wa kuwa na fungu la dharura.

2. Kiasi cha fedha unachopaswa kuwa nacho kwenye fungu lako la dharura.

3. Jinsi unavyoweza kuanza kuweka akiba hata kama kipato chako ni kidogo.

4. Jinsi ya kudhibiti matumizi yako.

5. Jinsi ya kuondoka kwenye madeni.

6. Jinsi unavyoweza kujijenga kifedha licha ya kuwa na wategemezi wengi.

7. Jinsi ya kuzuia ongezeko la kipato lisiongeze gharama za maisha.

8. Kwa nini elimu kubwa ni kikwazo kufikia uhuru wa kifedha.

9. Vitabu vitatu ambavyo kila mtu anayetaka kufanikiwa anapaswa kuvisoma.

10. Hatua tatu za uhakika za kufikia utajiri kutoka kwa Charlie Munger.

Karibu sana usikilize kipindi hiki cha redio, kuna mengi mno ya kujifunza kuhusu fedha na mafanikio kwa ujumla. Kusikiliza fungua; https://wp.me/p4VYpK-79q

Nichukue nafasi hii kukukaribisha kwenye KISIMA CHA MAARIFA, ambapo tutakuwa karibu na utapata nafasi ya kujifunza na kupata mwongozo sahihi wa kufikia mafanikio makubwa kwenye maisha yako. Kujiunga, tuma ujumbe wenye maneno KISIMA CHA MAARIFA, kwa wasap kwenda namba 0717396253 kisha utatumiwa maelekezo.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania