“Humanity has begun to understand that we will all rise or fall together—that we are bound together, as we live together. People are listening more and more to the voice which speaks this inside of us.” —LUCY MALORY
Kitu kimoja tunachopaswa kufahamu na kufanyia kazi ni kwamba sisi binadamu wote ni kitu kimoja.
Haijalishi rangi, utaifa, kabila au tofauti nyingine ya nje,
Kiroho sote ni kitu kimoja.
Na tutainuka au kuanguka kama kitu kimoja.
Msongo wa mawazo ni matokeo ya mtu kujifikiria mwenyewe na kusahau wengine.
Maumivu ni matokeo ya kushindana na wengine badala ya kushirikiana.
Kutokuelewana ni matokeo ya kudharau wengine na kuona hawana maana.
Ukitambua umuhimu wa kila mtu kwenye maisha yako, utakuwa na maisha bora na tulivu.
Kwa sababu, kila unachotaka kwenye haya maisha, utakipata kutoka kwa watu wengine.
Kama unafanya biashara, hutajiuzia mwenyewe kile unachouza, bali utawauzia wengine.
Hivyo kama hakuna wengine, hakuna biashara, huwezi kupata chochote unachotaka.
Kadhalika kwenye maeneo mengine kama kazi na mahusiano, tunawahitaji sana wengine.
Njia bora ya kwenda na wengine ni kuwapenda, kuwathamini na kuwaheshimu.
Msingi bora wa kuendesha maisha yako ni kutambua kwamba ili upate chochote unachotaka, unapaswa kwanza kuwasaidia wengine kupata kile wanachotaka.
Kwa maneno mengine, huwezi kufanikiwa kama hujawawezesha wengine nao kufanikiwa.
Acha ubinafsi wa kujiangalia wewe tu na anza kuwaangalia wengine,
Utaziona fursa nyingi za kuwasaidia, ambazo pia zitakusaidia wewe kupiga hatua.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania