Elliot alikuwa mfanyakazi mwenye nafasi na cheo kizuri kwenye moja ya kampuni kubwa sana. Maisha yake yalikuwa yenye mafanikio makubwa kwenye kila nyanja, kazi inayomlipa vizuri, uwekezaji unaomzalishia faida na familia yenye furaha. Hii ilifanya watu wengi watamani maisha yake, wengine wakimwangalia kama mtu wa mfano kwao, wakitamani kufika ngazi alizofika yeye.
Lakini Elliot alikuwa na tatizo moja, maumivu ya kichwa yasiyokoma. Yalianza kidogo kidogo na kuendelea kukua kadiri muda ulivyokwenda. Mwanzo alikuwa akitumia dawa za maumivu zinasaidia, lakini baadaye hata dawa za maumivu zilidunda, kichwa kilimuuma sawa.
Alienda hospitali na baada ya kufanyiwa vipimo vingi aligundulika kuwa na uvimbe kwenye ubongo wake, ambapo ulikua unakua kidogo kidogo na ndiyo ulisababisha kichwa kimuume sana. Njia pekee ya kutibu hilo ikawa upasuaji, ambao ulifanyika kwa mafanikio makubwa sana na Elliot akapona, matatizo ya kuumwa kichwa yakaisha kabisa.

Baada ya upasuaji, maisha ya Elliot yalibadilika sana, aliporudi kazini hakuwa tena mtu wa kujali majukumu yake na kuyatekeleza kama awali. Badala yake ilimchukua muda sana kukamilisha hata jukumu dogo. Kila jukumu alilopewa alishindwa kulimaliza kwa wakati. Kuna wakati alitumia muda mwingi kuamua nini afanye, au kuamua atumie kalamu ya rangi nyeusi au rangi ya bluu. Tabia zake mpya zilileta hasara kubwa kwenye kampuni na akaishia kufukuzwa kazi.
Nyumbani nako mambo hayakuwa mazuri, maisha ya Elliot yalikuwa na mabadiliko makubwa sana. Kitendo tu cha kuamka asubuhi ilikuwa shughuli kubwa kwake, na hata alipoamka, siku nzima alikaa kwenye kochi kuangalia tv. Hakujali chochote kuhusu mke wake wala watoto wake, kila siku alikuwa akifanya vitu vinavyowakwaza sana, huku yeye akionekana hajali. Mke wake alishindwa kuendelea na maisha yake, akisema huyo siyo Elliot aliyemjua, hivyo akamwacha.
Maisha ya Elliot yalizidi kwenda mrama, baada ya kufukuzwa kazi alianza kufanya uwekezaji ambao kila mtu alishangaa, aliwekeza maeneo ya hovyo na alitapeliwa kwa urahisi, na hivyo kupoteza mali zake nyingi. Baada ya kuachwa na mke, ndani ya muda mfupi alipata mwanamke mwingine, wakafunga ndoa bila ya kumjulisha mtu yeyote wa karibu yake, na baada ya ndoa mwanamke huyo akamwacha, huku akichukua nusu ya mali zake.
Ndani ya muda mfupi, Elliot alijikuta hana kazi, hana familia, hana mali na hana pa kuishi. Lakini hayo yote hakujali. Ndipo kaka yake alipoona kuna kitu hakipo sawa, na kuchukua hatua ya kutafuta madaktari wa kujua ndugu yake ana shida gani.
Ni katika kutafuta tatizo na njia ya kumsaidia Elliot, ndipo walipokutana na Antonio Damasio ambaye ni daktari bingwa wa ubongo na mishipa ya fahamu. Antonio alimfanyia kila kipimo Elliot na vipimo vyote vilionesha hana tatizo kabisa. Alijaribu kumuuliza maswali mbalimbali kupima uelewa wake, akagundua ana uelewa mkubwa mno wa kila kinachoendelea, hakuna swali lililomshinda.
Kwa kusikia yale aliyopitia, Antonio alishawishika kwamba Elliot ana shida. Ili kuijua alimuuliza aelezee yale yote aliyofanya kwenye maisha yake mpaka alipofika sasa, na kwa nini aliyafanya. Elliot aliweza kuelezea vizuri kila alichofanya, ila hakuweza kuelezea kwa nini alifanya aliyofanya.
Hapo ndipo Antonio aliona shida ya Elliot iko wapi, alifanya vipimo vya kichwa na kugundua kwamba, upasuaji wa kuondoa uvimbe aliofanyiwa, uliondoa pia sehemu ya ubongo wake wa mbele, ambayo ni sehemu inayohusika na hisia.
Hivyo Elliot hakuwa na hisia zozote na hilo ndiyo lilibadili maisha yake. Hakuweza kufanya maamuzi sahihi kwake, ndiyo maana alichukua muda mwingi kufanya kitu, hakuweza kupima hatari ya vitu ndiyo maana alipoteza kila kitu.
Kupitia Elliot na wagonjwa wengine, Antonio aligundua kitu kikubwa sana, kwamba bila ya hisia, hatuwezi kupiga hatua yoyote kwenye maisha yetu. Japo tumekuwa tunaona hisia kama kikwazo kwetu, lakini bila ya hisia, sisi siyo chochote.
Na hili linadhibitisha kwamba sisi binadamu ni viumbe wa hisia, ambapo tunafanya maamuzi yetu kwa hisia na kisha kuyahalalisha kwa fikra. Kama ukiwa na fikra pekee bila ya hisia, huwezi kufanya maamuzi sahihi. Na ukiwa na hisia pekee bila fikra, utafanya mambo ambayo ni hatari sana.
Hivyo ili tufanikiwe, tunahitaji fikra na hisia, vyote vifanye kazi kwa pamoja. Na hapo ndipo mchago wa hamasa kwenye mafanikio yetu unapoingia.
Kumekuwa na wimbi kubwa la watu ambao wanabeza mchango wa hamasa (motivation) na wahamasishaji (motovational speakers) kwamba ni vitu vya uongo au utapeli. Lakini hilo siyo sahihi, hamasa ni kiungo muhimu sana kwa mafanikio yetu, na hivyo wale wanaotupa hamasa, ni watu wa kuwathamini sana.
Watu wengi wamekuwa wakibeza hamasa na wahamasishaji kwa sababu wamekuwa hawaelezi kwamba hamasa peke yake haiwezi kukupa mafanikio. Ni lazima uchukue hatua kwa hamasa uliyopata, la sivyo hamasa hiyo itakuwa kitu cha kujiliwaza na kujidanganya.
Lakini pia watu wengi wanaohamasisha wamekuwa kikwazo kwa sababu maisha yao hayaakisi kile wanachohamasisha. Wengi huongeza chumvi kwenye hamasa wanazotumia kwa wengine, kitu ambacho kinawafanya wanaopokea hamasa hizo kuwa na wasiwasi kuhusu usahihi wake.
Lakini pamoja na changamoto hizo za wahamasishaji, wewe usiingie kwenye mkumbo wa wale wanaobeza hamasa na wahamasishaji, badala yake tafuta njia bora itakayokuwezesha kupata hamasa na kupiga hatua zaidi.
Karibu upate hamasa kila siku itakayokusaidia kupiga hatua na kufanikiwa.
Aliyekuwa mhamasishaji mashuhuri, Zig Zigler aliwahi kuhojiwa kwamba amekuwa anasisitiza watu kujihamasisha kila siku. Akajibu ndiyo, na kueleza kwamba hamasa ni kama kula au kuoga, huli mara moja ukashiba milele, au kuoga mara moja ukatakata milele. Unakula kila siku na kuoga kila siku, hivyo pia unahitaji hamasa kila siku. Aliendelea kusema dunia imejaa mambo mengi ya kukatisha tamaa kiasi kwamba kama huna njia ya kuhamasika kila siku, huwezi kufanya makubwa.
Rafiki yangu mpendwa, napenda kuchukua nafasi hii kukukaribisha kwenye huduma ambayo itakupa wewe nafasi ya kuhamasika kila siku. Huduma hiyo ni KISIMA CHA MAARIFA. Kwa kuwa ndani ya KISIMA CHA MAARIFA, kila siku unapata mafunzo yanayokupa maarifa na hamasa ya kuchukua hatua. Lakini pia unakuwa umezungukwa na watu wengine wenye kiu ya mafanikio na ambao wanachukua hatua kuyafikia. Hivyo unakuwa kwenye mazingira ya tofauti kabisa na jamii zetu zilivyo, na hilo linakupa hamasa na msukumo mkubwa wa kuchukua hatua ili kufanikiwa.
Rafiki, jua kabisa kwamba safari ya mafanikio siyo rahisi, na peke yako utakutana na vikwazo vingi. Unahitaji kuwa eneo ambalo litakupa nguvu ya kupambana na vikwazo hivyo. Katibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA kwa maelezo yanayopatikana hapo chini, yasome mpaka mwisho.
KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.
KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi.
Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;
1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.
2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)
3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.
4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.
5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.
6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.
7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.
8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.
9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.
10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.
Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.
Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.
Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.
Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.
Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail
Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.
Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania