“The improvement of society can be achieved only by the moral improvement of individuals.” – Leo Tolstoy
Msukumo mkuu kwetu kufanya chochote kile ni yale manufaa tunayoyapata.
Hasa pale kitu hicho kinapokuwa kigumu au kinachotugharimu wakati wa kufanya.
Huwa tunaangalia ni manufaa gani ambayo tunayapata.
Huwa hatukubali kuteseka mpaka tuwe na uhakika kuna manufaa tunayapata.
Japo hakuna ubaya kwenye kufikiri hivyo, unapaswa kutanua zaidi kufikiri kwako.
Unapaswa kuuona ukweli kwamba chochote kizuri unachokifanya, japo ni kwa manufaa yako, lakini pia kina manufaa makubwa kwa jamii nzima.
Unapokazana kuwa mtu bora, mwenye maadili na misimamo sahihi,
Jamii inanufaika zaidi, kwa sababu unaongeza idadi ya watu bora, unakuwa mfano kwa wengine nao kuwa bora na pia unawafundisha wengine wawe bora pia.
Kama umekuwa na tabia zisizo sahihi na ukaziacha kwa kujijengea tabia sahihi,
Wewe utanufaika sana kwa tabia bora ulizojijengea,
Lakini pia jamii itanufaika zaidi kwa sababu imepunguza mtu mmoja aliyekuwa mzigo kwa tabia zake na imeongeza mtu mmoja ambaye ana mchango mzuri kwa jamii nzima.
Ni wajibu wetu kila siku kukazana kuwa bora zaidi,
Siyo kwa sababu tutanufaika sana, bali pia kwa sababu jamii itanufaika sana kwa sisi kuwa bora.
Kwa kuifikiria jamii hivi, kunakupa msukumo mkubwa wa wewe kuwa bora zaidi.
Kwa kuwa unajua siyo kwa ajili yako pekee.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania