Rafiki yangu mpendwa,

Tangu enzi na enzi kumekuwepo na matapeli hapa duniani, lakini bado watu wamekuwa hawajifunzi na kuondokana na hali za kutapeliwa.

Huwa ni vigumu sana kuepuka kutapeliwa kwa sababu matapeli wanaijua vizuri saikolojia wa binadamu.

Hivyo huwa wanacheza na saikolojia hiyo kuhakikisha wanakunasa kwenye mpango wao wa utapeli, huku ukishindwa kuona wazi kwamba ni utapeli.

Na utapeli siyo lazima uibiwe kitu, hata kitendo cha kushawishiwa kitu fulani ni fursa, ukahamasika na kuingia kisha kugundua siyo fursa kama ulivyokuwa unafikiria, ni utapeli tosha.

Hakuna eneo ambalo wengi wameyumbishwa na kudanganywa kama kwenye fursa mpya. Kila siku kuna kitu kipya watu wanaibuka nacho, wakidai kinaleta mafanikio makuba bila ya kufanya kazi.

Kwa kuwa saikolojia yetu binadamu ni kupenda urahisi, kutaka kupata mafanikio makubwa bila ya kufanya kazi, inakuwa rahisi kunasa kwenye mitego kama hiyo.

Mbaya zaidi, mitego ya matapeli huwa ni migumu sana kuikwepa, hata kama ulishatapeliwa tena na mtu huyo huyo, anaweza kuja kwako tena, akiwa na utapeli mwingine na kukuambia huu ni tofauti na ule wa mwanzo. Unakubali, unaingia na kuumizwa tena

Leo tunakwenda kujifunza msimamo sahihi wa kuishi ili uweze kupata mafanikio makubwa na uepuke kutapeliwa na wengine. Kwa kuwa na msimamo huu, siyo tu utaepuka kutapeliwa, bali pia utaweza kufanya kile kilicho sahihi na kinachokupa mafanikio makubwa.

Karibu ujifunze msingi mkuu wa maisha ya mafanikio.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tunao msimamo mkuu wa maisha ya mafanikio ambao tunauishi kila siku.

Msimamo huo mkuu una maneno matatu; KAZI, UPENDO NA HUDUMA. Haya ni maeneo matatu ambayo ukiyasimamia vizuri lazima utapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako. Haijalishi unaanzia wapi au uko kwenye mazingira gani, hakuna anayesimamia hayo na kubaki pale alipo au kutapeliwa na wale wenye tamaa.

KAZI.

Kazi ndiyo msingi mkuu wa mafanikio yoyote yale, hakuna chochote unachoweza kupata bila ya kuweka kazi.

Hakuna kitu chochote kinachopatikana bure bila ya kuweka kazi, ni lazima uwe tayari kuweka kazi kama unataka kupata kile unachotaka.

Pia kadiri unavyotaka kupata mafanikio makubwa zaidi, ndivyo unavyohitajika kufanya kazi zaidi.

Kutumia kazi kama msimamo, usijihusishe na kitu chochote ambacho hakikutaki wewe uweke kazi.

Yaani mtu anapokuja kwako na kukuambia kuna fursa ya kupata mafanikio makubwa bila ya kufanya kazi, kimbia haraka sana, hapo unakwenda kutapeliwa.

Nakuambia kimbia haraka kwa sababu ukiendelea kusikiliza, utaanza kujiambia labda safari hii ni tofauti, wacha tu ni jaribu kwa sababu huwezi kupata bila kupoteza. Huko kujishawishi kwako ndiko kunawarahisishia matapeli kazi zao.

Nenda na msimamo huu, kuwa mkali sana kwenye huu msimamo na usitetereke, ukisikia ni mafanikio bila kazi, wala usiulize huo mpango ukoje, sema asante na ondoka haraka sana, huna hata haja ya kuaga.

Unachopaswa kuzingatia cha kwanza kabisa ni kazi, ndiyo unataka mafanikio, lakini je ni kazi gani unapaswa kuifanya ili upate mafanikio hayo? Kama unaahidiwa hakuna kazi ya kufanya, wewe unapanda fedha zako, unaenda kutulia nyumbani na baada ya muda mfupi unakuja kuvuna faida mara mbili, chagua kuzipenda pesa zako na ukimbie la sivyo matapeli watazipenda zaidi.

Na hata kama ni mpango wa uwekezaji, lazima uone jinsi fedha hizo unazowekeza zinaenda kufanya kazi, siyo unaambiwa weka fedha upate mara mbili, zinakujaje mara mbili, kwa aina ipi ya kazi yenye marejesho makubwa hivyo kwa muda mfupi? Hujui, hapo unaishia kutapeliwa.

UPENDO.

Unapokuwa unaanzia kwenye umasikini mkubwa, huwa kipaumbele chako cha kwanza ni kupata fedha, unapataje fedha hizo siyo muhimu sana kwako. Unakuwa tayari kufanya chochote kinachokuingizia fedha, kwa sababu unazihitaji sana, kwa sababu fedha kwako ni jambo la maisha na kifo.

Lakini kadiri unavyoendelea kujijengea utajiri, unagundua kwamba kadiri unavyopata fedha zaidi, ndivyo zinavyokuwa hazina mchango kwenye furaha yako.

Katika hali hiyo, kitu pekee kinachoweza kukupa furaha ni kile unachofanya, na siyo fedha unazopata.

Lakini pia furaha zaidi utaipata kutoka kwa wale wanaokuzunguka na wale ambao kile unachofanya kinawasaidia.

Kama ni mwalimu, unapofundisha na watu wakaelewa, wakaja kukushukuru kwa jinsi umeyafungua maisha yao, hilo litakupa furaha kuliko fedha ulizopata.

Hivyo msimamo mwingine muhimu kujiwekea kwenye kile unachofanya ni UPENDO. Unapaswa kupenda sana kile unachofanya na kuwapenda wale unaowalenga kwenye kile unachofanya.

Siyo lazima uwe umezaliwa ukiwa unapenda kitu hicho, hakuna anayezaliwa akiwa anapenda chochote zaidi ya kunyonya. Unachopaswa ni kuchagua kufanya kile unachopenda au kupenda kile unachofanya na kuwapenda wale unaowalenga.

Kwa msimamo huu wa upendo, matapeli hawawezi kukunasa kwenye mitego yao, kwa sababu mtego wao mkuu ni tamaa ya kupata fedha haraka, bila kuangalia unazipataje. Wewe kwa msimamo wako, kipaumbele cha kwanza kwako ni kufanya unachopenda na kuwapenda wale unaowalenga.

Mipango ya kitapeli inakosa sifa hizo na hivyo haiwezi kukunasa wewe.

Tanguliza upendo kwa kila unachofanya na upendo kwa wale unaowalenga na hiyo itakuwa kinga nzuri kwako dhidi ya utapeli.

HUDUMA.

Watu wengi ni rahisi kutapeliwa kwa sababu wao wanachoangalia ni kimoja, wanapata nini.

Huwa hawapati nafasi ya kujiuliza je kile wanachofanya kinawanufaishaje wengine, wanachoangalia ni wao binafsi wananufaikaje.

Sasa mipango yote ya kitapeli huwa haina manufaa kwa wengine, kwa kuwa huwa haina inachofanya zaidi ya kutapeli fedha.

Hivyo huwa inalenga kuibua tamaa ndani ya mlengwa, ikimwonesha kwamba atanufaika sana.

Kama unataka usitapeliwe tena kwenye maisha yako, ishi kwa msimamo wa HUDUMA, kwa msimamo huo, usitegemee kupata chochote kama hujawasaidia wengine kupata kile wanachotaka.

Chagua kuwa mtu wa huduma, kuwa mtu unayekazana kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi kupitia kile unachofanya, kwa sababu unajua maisha ya wengine yakiwa bora, basi na maisha yako pia yatakuwa bora.

Rafiki yangu mpendwa, hayo ndiyo maeneo matatu ya kuzingatia kwenye msimamo mkuu wa maisha ya mafanikio, KAZI, UPENDO NA HUDUMA. Zingatia maeneo hayo matatu kila siku na kila mahali, na hakuna mtu yeyote, hata awe mjanja kiasi gani atakayeweza kukutapeli.

Kwa kila fursa mpya inayokuja kwako, jiulize maswali haya matatu na upate majibu ya ndiyo kwenye maswali hayo kabla hujaanza hata kufikiria kuifanya.

1. Je fursa hii inanitaka mimi kufanya kazi, niweke juhudi ili kupata manufaa ninayoahidiwa kupata?

2. Je ninapenda kile ninachokwenda kufanya na wale ninaowalenga?

3. Je fursa hii ina mchango wa kuyafanya maisha ya wengine kuwa bora zaidi?

Kama kuna jibu lolote limekuja HAPANA, kimbia haraka, hakuna fursa hapo, kuna utapeli.

Karibu kwenye mazingira yatakayokuwezesha kuishi msingi huo kila siku.

Rafiki yangu mpendwa, tunaishi kwenye jamii ambazo hakuna tena watu wanaoishi kwa misingi yoyote. Kila mtu anasukumwa na tamaa ya kupata zaidi ya wengine.

Hata wale ambao unawaamini kama watu sahihi kwako kukushauri, wanakuwa wa kwanza kukuingiza kwenye michezo ya kitapeli.

Hivyo ni vigumu sana kuweza kuishi misingi hii, hasa pale jamii nzima inayokuzunguka inapokuwa haina misimamo hiyo. Kwa kuwa kwenye jamii ya aina hiyo ni rahisi kuangukia kwenye utapeli, kwa sababu matapeli watakuambia wengine wote wamechukua fursa hii, umebaki wewe tu. Na hapo utaanza kujidanganya, haiwezekani watu wote hao wawe wamekosea na mimi nimepatia, hata hivyo kifo cha wengi ni harusi. Unajidanganya, unaingia na kuishia kupoteza kama wengine wengi wanavyopoteza.

Kuna mazingira yanayokuwezesha kuishi msimamo huu wa mafanikio kila siku, bila ya kuacha, kuchoka au kukatishwa tamaa.

Mazingira hayo ni KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI inayokupa nafasi ya kufikiri kwa kina na kuianza siku yako ukiwa na mtazamo sahihi. Pia katika tafakari hiyo unapata nafasi ya kujikumbusha msimamo huu muhimu wa mafanikio. Hivyo hautaianza siku kabla hujajikumbusha KAZI, UPENDO NA HUDUMA, hivyo hata atakapokuja mtu kwako na fursa mpya, utajikumbusha umeianza siku yako kwa tafakari na kuitathmini fursa hiyo kabla hujaingia kichwa kichwa.

Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA unazungukwa na watu wengine ambao wanaishi msimamo huu mkuu wa mafanikio hivyo hilo linakupa na wewe hamasa ya kuishi kuwa na msimamo huo pia. Unapokuwa pekee kwenye eneo ambalo hakuna anayeishi misimamo hii inakatisha tamaa, lakini unapozungukwa na wengine wanaoishi misimamo hiyo, inakupa moyo wa kuendelea kuiishi misimamo hiyo.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Unajiweka kwenye hatari ya kuendelea kutapeliwa na utapoteza fedha nyingi kwenye utapeli kuliko ada kidogo utakayolipa na kuwa mwanachama.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kuishi misimamo huu muhimu wa mafanikio na uweze kuepuka kutapeliwa ili uwe na mafanikio makubwa na yatakayodumu kwa muda mrefu.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania