Rafiki yangu mpendwa,

Hapo zamani za kale, watu walikuwa wakijenga nyumba zao bila ya kuweka msingi imara. Walitumia zana zilizopatikana pale walipo, iwe ni miti, mawe, mchanga na kadhalika.

Waliweka kuta za kuweza kujisitiri, na mambo yalikwenda vizuri. Lakini walijifunza kitu muhimu sana ambacho kiliwaumiza na kuwapa somo la kufanyia kazi.

Kipindi ambacho kuna utulivu, nyumba zao zilikuwa vizuri. Lakini kipindi ambacho siyo cha utulivu, kama wakati wa upepo mkali, mvua nyingi na matetemeko, nyumba zao zilibomoka na hivyo kujikuta hawana pa kukaa.

Hapo ndipo watu walipojifunza kwamba nyumba bila ya msingi, haiwezi kuhimili changamoto mbalimbali za kimazingira. Na kadiri nyumba inavyokuwa kubwa, ndivyo msingi wake unapaswa kuwa imara.

Hadithi hii inaendana sana na maisha yetu ya kila siku, watu wote tunazaliwa tukiwa tuna fanana, lakini kadiri tunavyokua, tofauti zinajengeka ndani yetu. Tunapofikia utu uzima ambapo tunapaswa kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo kwenye maisha, wapo wanaoweza kuzikabili na kuwa bora na wapo ambao changamoto zinawapoteza kabisa.

Kinachowatofautisha wale wanaoweza kukabiliana na changamoto mbalimbali na kufanikiwa, na wale ambao wanashindwa ni misingi ambayo watu hao wanayo au wameikosa.

Kama ilivyo kwa nyumba, watu wanaofanikiwa ni wale ambao wana msingi wanaosimamia, msingi ambao unawazuia wasitetereshwe na chochote kile. Na kadiri mtu anavyopata mafanikio makubwa, ndivyo msingi wake unakuwa imara zaidi.

Hivyo rafiki yangu, kama umefika mahali na kuona maisha yanakuchapa kila kona, kama kila unachojaribu unashindwa na kama unaona wengine mambo yao ni rahisi ila kwako tu ndiyo mambo magumu, napenda nikuhakikishie jambo moja, tatizo ni misingi.

Huenda huna misingi kabisa, au misingi uliyonayo siyo sahihi.

Kama umekuwa unalalamikia kwamba kipato chako hakitoshelezi,

Kama umekuwa unajiambia huna muda wa kutosha kufanya yale unayotaka kufanya,

Kama umekuwa unapanga kufanya vitu lakini unaahirisha,

Kama umekuwa msemaji sana kuliko mfanyaji,

Na kama upo kwenye kazi au biashara kwa miaka mingi ila hakuna hatua kubwa unazopiga,

Tatizo ni moja, huna misingi kabisa au misingi uliyonayo siyo sahihi.

Na haijalishi utahangaika kiasi gani, haijalishi utalalamika au kulaumu watu gani, hutaweza kutoka hapo ulipo bila ya kujijengea misingi sahihi na kuifuata mara zote.

Karibu ujifunze msingi mkuu wa maisha ya mafanikio.

Kwenye KISIMA CHA MAARIFA, tunao msingi mkuu wa maisha ya mafanikio ambao tunaufuata na kuuishi kila siku.

Msingi huo mkuu una maneno matatu; NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Haya ni maeneo matatu ambayo ukiyazingatia lazima utapiga hatua kubwa sana kwenye maisha yako. Haijalishi unaanzia wapi au uko kwenye mazingira gani, hakuna anayesimamia hayo na kubaki pale alipo.

NIDHAMU.

Nidhamu ndiyo kikwazo cha kwanza kwa wengi kufanikiwa. Watu wengi hawana nidhamu, wanaendesha maisha yao kwa hisia na siyo mipango. Wanapanga mambo mengi lakini hawayafanyi kwa sababu hawana nidhamu.

Hivyo kama unataka kupata mafanikio makubwa, eneo la kwanza kufanyia kazi ni nidhamu.

Ili uweze kufikia mafanikio makubwa, kuna nidhamu nne muhimu sana unazopaswa kujijengea na kuziishi kila siku.

Moja ni NIDHAMU BINAFSI, hapa ni kuwa na nidhamu kwako mwenyewe na kuweza kujisimamia kwa umakini bila ya kujionea huruma. Chochote unachopanga kufanya, fanya kama ulivyopanga, bila ya kuruhusu chochote kikuzuie.

Mbili ni NIDHAMU YA FEDHA, hii ndiyo itakayokufikisha kwenye uhuru wa kifedha na utajiri. Muhimu kuzingatia hapa ni matumizi yako hayapaswi kuzidi kipato chako, na kwa kila kipato, weka akiba ambayo baadaye utaiwekeza sehemu inayozalisha zaidi.

Tatu ni NIDHAMU YA MUDA, kwenye zama tunazoishi sasa, zama ambazo mambo ya kufanya ni mengi lakini muda tulionao ni mchache, unapaswa kuweka vipaumbele vyako na kuvisimamia hivyo. Jua muda wako ni wa uhaba sana, usiruhusu upotee kwa mambo yasiyo muhimu. Kuwa bahili wa muda wako, utumie kwa yale muhimu pekee.

Nne ni NIDHAMU YA KAZI, jiwekee viwango vyako vya ufanyaji wa kazi na kazana kufikia viwango hivyo kila siku, tenga muda wa kazi na utumie kufanya kazi. Kazi zako ziwe za viwango vya juu na yeyote akiona ulichofanya, akiri kweli kazi imefanyika.

Ukikazana kujijengea nidhamu hizi na kuziishi kila siku, hakuna namna utaacha kufanikiwa.

UADILIFU.

Kila siku tunasikia hadithi za watu waliokuwa wamefanikiwa na baadaye kuyapoteza mafanikio yao. Labda ni mtu aliyekuwa tajiri mkubwa lakini akaishia kupoteza utajiri wote.

Mambo hayo huwa hayatokei kwa bahati mbaya, bali huwa yanasababishwa. Na kwa wale ambao walikuwa wamefanikiwa sana, na wakaanguka kiasi cha kutoweza kuinuka tena, tatizo huwa linaanzia kwenye uadilifu.

Unakuta kwenye njia walizotumia kupata mafanikio yao makubwa, hazikuwa sahihi, kuna mambo waliyofanya ambayo hayakuwa sahihi. Japokuwa mambo hayo yaliwalipa kwa wakati huo, lakini yalitengeneza deni, ambalo wamekuja kulilipa kwa kupoteza kila kitu.

Usijaribu kabisa kutumia njia isiyo sahihi kufanikiwa, hata kama umeona wengine wamefanikiwa kwa njia hiyo, jua ni swala la muda tu. Huwezi kuiibia asili na wala asili haiwezi kukuibia, huwa inalipa kila kitu kwa usawa.

Msingi wa uadilifu ni muhimu sana kama unataka kujenga mafanikio yatakayodumu kwa muda mrefu. Unaweza kuchelewa kuyapata, lakini yatadumu. Wenzako wanaweza kuyapata haraka kwa njia zisizo sahihi, lakini wakayapoteza haraka pia.

Kuwa mwadilifu kwa kufanya kilicho sahihi mara zote, hata kama hakuna anayekuona, hata kama inapelekea kupoteza kitu fulani, uadilifu ni kitu unachopaswa kukisimamia kwa gharama yoyote ile.

Tunaishi kwenye jamii ambayo uadilifu umeshuka sana, kila mtu anatafuta njia ya kupata anachotaka, iwe ni sahihi au la. Ndiyo maana wizi, utapeli, rushwa na hata matumizi mabaya ya madaraka ni vitu vinavyoshamiri. Wewe ukijijengea msingi wa uadilifu, kwa kufanya kile kilicho sahihi mara zote, utajenga mafanikio yatakayokupa amani na yatakayodumu kuliko ya wengine.

KUJITUMA.

Jamii imekuwa inakudanganya kwamba unapaswa kupokea kwanza kabla hujatoa. Nasema imekuwa inatudanganya kwa sababu ni sawa na kuchukua kuni kisha kuziweka jikoni na kuziambia nipe moto. Au kwenda shambani na kuliambia shamba nipe mazao.

Wote tunajua hivyo sivyo mambo yanavyokwenda, kabla kuni hazijakupa moto, lazima wewe uzipe moto kwanza. Kabla shamba halijakupa mazao, lazima upande mbegu kwanza. Ni kanuni ya asili, huwezi kwenda kinyume nayo na ukabaki salama.

Sasa angalia jinsi wengi wanakwenda kinyume na kanuni hiyo ya asili, halafu wanashangaa kwa nini hawafanikiwi.

Mtu yupo kwenye kazi miaka mingi, na kipato anacholipwa ni kidogo, na anachojiambia ni hiki, wakiniongezea mshahara ndiyo na mimi nitafanya kazi zaidi. Kwa mtazamo huo, anajikuta akibaki na mshahara huo huo kwa miaka mingi. Njia sahihi siyo kusubiri uongezewe mshahara ndiyo ufanye kazi zaidi, bali unapaswa kufanya kazi zaidi ya unavyofanya sasa, na hapo utajiweka kwenye mazingira ya kulipwa zaidi.

Kadhalika kwenye biashara, utakuta mtu yupo kwenye biashara miaka mingi lakini hakuna hatua kubwa anazopiga. Hiyo ni kwa sababu mtazamo wake ni huu; nikipata wateja bora nitawahudumia vizuri. Kinachotokea ni anabaki na wateja wa hovyo kwa sababu hawahudumii vizuri. Kama unataka wateja bora, anza kwa kutoa huduma ambazo ni nzuri kuliko zinazopatikana maeneo mengine.

KUJITUMA ni pale unapofanya zaidi ya unavyotegemewa kufanya na hilo ni hitaji muhimu sana kwenye mafanikio yako. Hakuna yeyote aliyefanikiwa ambaye amekuwa anafanya kile anachotegemewa kufanya, bali wamekuwa wakifanya zaidi ya wanavyotegemewa kufanya.

Kwa chochote unachofanya, nenda hatua ya ziada, hata kama huoni ni namna gani utalipwa zaidi, wewe fanya zaidi. Na kama nilivyokuambia, kanuni ya asili huwa inafanya kazi, chochote unachotoa, lazima kitarudi kwako.

Unaweza usilipwe zaidi na yule aliyekuajiri sasa, lakini kuna mtu ataona juhudi zako na atakupa fursa nzuri zaidi. Wateja ulionao sasa wanaweza wasijali kile cha ziada unachowafanyia sasa, lakini kuna wengine wataona na kuvutiwa kufanya biashara na wewe.

Hivyo kujituma hakuwanufaishi wengine pekee, bali kunakunufaisha na wewe pia. Hivyo kwa kila unachofanya, jitume, nenda hatua ya ziada, fanya zaidi ya unavyotegemewa kufanya.

Rafiki yangu mpendwa, hayo ndiyo maeneo matatu ya kuzingatia kwenye msingi mkuu wa maisha ya mafanikio, NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA. Zingatia maeneo hayo matatu kila siku na kila mahali, na hakuna kitakachoweza kukuzuia usifanikiwe.

Karibu kwenye mazingira yatakayokuwezesha kuishi msingi huo kila siku.

Rafiki yangu mpendwa, maisha yetu ya kila siku yana changamoto nyingi, kwa kifupi tunaweza kusema yanavuruga sana. Unaweza kuianza siku ukiwa na nia njema, ukiwa umejipanga kweli kwenda kuiishi kwa NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA.

Lakini siku nzima ikavurugika, ulipanga ufanye vitu fulani, uliotegemea kufanya nao wanakuangusha hivyo hufanyi (NIDHAMU imeanguka), ulitegemea ufanye kilicho sahihi, mtu anakuambia kuna fursa ya kujinufaisha zaidi na kila mtu anaitumia, ni wewe tu hujanufaika, unaona bora na wewe uitumie (UADILIFU umepotea). Unaamua kufanya zaidi ya unavyotegemewa, lakini wenzako wanakuambia acha kiherehere, hakuna anayeona wala kujali, hivyo unaamua uendelee kufanya kawaida (KUJITUMA kunapotea).

Ukienda hivyo kwa siku chache, unasahau kabisa msingi huo mkuu na kurudi kwenye maisha ya kawaida, na utajikuta unasota miaka na miaka bila ya kupiga hatua yoyote.

Kuna mazingira yanayokuwezesha kuishi msingi huu wa mafanikio kila siku, bila ya kuacha, kuchoka au kukatishwa tamaa.

Mazingira hayo ni KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI inayokupa nafasi ya kufikiri kwa kina na kuianza siku yako ukiwa na mtazamo sahihi. Pia katika tafakari hiyo unapata nafasi ya kujikumbusha msingi huu muhimu wa mafanikio. Hivyo hautaianza siku kabla hujajikumbusha NIDHAMU, UADILIFU NA KUJITUMA, hivyo hata kama utatetereka siku moja, siku inayofuata utajikumbusha na kufanya kilicho sahihi.

Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA unazungukwa na watu wengine ambao wanaishi msingi huu mkuu wa mafanikio hivyo hilo linakupa na wewe hamasa ya kuishi misingi hii. Unapokuwa pekee kwenye eneo ambalo hakuna anayeishi misingi hii inakatisha tamaa, lakini unapozungukwa na wengine wanaoishi misingi hiyo, inakupa moyo wa kuendelea kuiishi misingi hiyo.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kuishi msingi huu muhimu wa mafanikio na uweze kufurahia mafanikio yatakayodumu kwa muda mrefu.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania