“As soon as I have a deadline, I work much better. Time unbounded is hard to handle.” — May Sarton
Unapokuwa na muda mwingi, muda usiokuwa na ukomo, badala ya kuwa manufaa kwako, unageuka kuwa sumu kwako.
Upo usemi kwamba ukitaka kitu kifanyike, mpe mtu ambaye hana muda, huyo atakifanya kweli.
Lakini ukimpa yule ambaye anakuambia ana muda mwingi, hatakifanya kwa wakati.
Ni asili yetu binadamu kusukumwa kuchukua hatua pale kitu kinapokuwa kwa uhaba.
Na ndivyo pia ilivyo kwenye muda,
Unapokuwa na muda mwingi, hupati msukumo wa kufanya kitu, unaona muda unao, na hivyo unaanza kuupoteza.
Unapogundua huna muda mwingi unaanza kuuthamini muda na hivyo unafanya kwa haraka zaidi.
Kwa kulijua hili, unapaswa kubadili jinsi unavyoweka mipango yako.
Chochote unachopanga kufanya, jiwekee muda wa ukomo, kwamba baada ya muda huo kuisha, hutakifanya tena, hata uweje.
Ukishakuwa na muda wa ukomo, akili yako itatulia kwenye kile ulichopanga kufanya.
Acha kabisa mazoea ya kupanga kufanya kitu bila kuweka ukomo wa muda.
Na hakikisha ukomo unaojiwekea unautekeleza kweli.
Kwa vitu ambavyo tayari vina ukomo, wewe jiwekee ukomo wa peke yako.
Labda una siku 10 za kukamilisha kitu fulani, wewe jiwekee ukomo wa siku 5.
Hilo litakusukuma kufanya na kumaliza mapema,
Na utaweza kukamilisha ndani ya muda,
Utakuwa mmoja kati ya wachache sana wanaofanya mambo yao kwa muda,
Na hilo litakupa sifa kubwa.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania