Rafiki yangu mpendwa,

Hakuna mtu ambaye hapendi mafanikio kwenye maisha yake.

Kila mmoja wetu anapambana kwa namna mbalimbali ili kuweza kupata mafanikio, kuwa na maisha bora kabisa yatakayomfanya afurahie kuwa hai.

Lakini kwenye kila jamii, wale wanaofanikiwa ni wachache sana kuliko wanaoshindwa.

Ukienda kwenye jamii yoyote ile na kuwachagua watu 100, 10 kati yao watakuwa na mafanikio makubwa kuliko wale 90 waliobaki. Lakini pia kuna kitu kitakushangaza, mtu mmoja katika hao 100 atakuwa na mafanikio makubwa kuliko wale 99 waliobaki.

Hapa unaweza kujiuliza kwa nini hilo linakuwa hivyo, nini kinawatofautisha wachache sana wanaofanikiwa na wengi wanaoshindwa?

Unaweza kusema ni elimu, lakini ukichunguza unagundua wanaofanikiwa sana wala hawana elimu kubwa sana.

Unaweza kusema ni juhudi wanazoweka, lakini unapoangalia unagundua wasiofanikiwa nao wanajituma sawa na waliofanikiwa.

Kwa kuona sababu ulizozoea hazikubaliani na hali hiyo, unajiambia basi kinachowatofautisha ni bahati. Kwamba waliofanikiwa wamekutana na bahati ambayo walioshindwa hawajaipata. Lakini hili pia si kweli, tukiangalia wale wanaokutana na bahati zinazojulikana wazi kama kushinda bahati nasibu, huwa hawapigi hatua yoyote kubwa kwenye maisha yao, zaidi ya kuanguka zaidi.

Watu kwa kutokujua nini hasa kinachowatofautisha wanaofanikiwa na wanaoshindwa, wamekuwa wanajizuia wenyewe kufanikiwa. Kwa sababu wanaishia kufanya yale ambayo yanawazuia zaidi wasifanikiwe.

Kikwazo kikuu kwa mafanikio.

Kikwazo kikubwa kwa mafanikio ya wengi ni kutokuamua kweli ni nini hasa wanachotaka kwenye maisha yao.

Kwa tafiti nyingi nilizofanya na vitabu vingi vilivyosoma nimekuwa naona hili likijirudia sana, kwamba ili ufanikiwe, lazima uamue ni kitu gani hasa unachokitaka, na kisha kupambana nacho bila kukata tamaa mpaka ukipate.

Kwenye moja ya vitabu ambavyo huwa nashauri kila mtu akisome, THINK AND GROW RICH, wameita hiyo DEFINITENESS OF PURPOSE yaani kulijua hasa kusudi lako na kuliishi hilo.

Kwenye kitabu hicho tunapewa mfano wa mama mmoja aliyemtuma mtoto wake aende kwa tajiri fulani kudai fedha yake na kumwambia asirudi mpaka ampe fedha hiyo.

Mtoto huyo akaenda, baada ya kumwambia tajiri yule kilichomleta, alimjibu aondoke kwani hawezi kumpa kwa sasa. Mtoto akamjibu hataweza kuondoka mpaka atakapopewa fedha hiyo. Tajiri huyo alimpigia kelele na kumtisha kwamba asipoondoka atamwadhibu vibaya. Lakini mtoto yule hakuondoka.

Baada ya muda, tajiri yule aliona dawa ni amlipe tu ili aondoke zake, kweli akamlipa na mtoto huyo akaondoka. Lakini hilo lilimfanya atafakari sana, ni nguvu gani imemfanya mtoto huyo amshinde? Na hapo alipata jibu ambalo naye alilifanyia kazi kwenye maisha yake na likamsaidia kufanikiwa zaidi.

Jibu alilolipata ni kwamba mtoto yule alijua nini anataka na hakuwa tayari kuondoka kabla hajapata kile anachotaka. Alikuwa king’ang’anizi hasa katika kuhakikisha anapata kile anachotaka.

Hiki ndiyo watu wengi wanachokikosa sasa.

Wanaweka juhudi kweli, lakini ni juhudi ambazo hazidumu eneo moja.

Leo mtu anasikia watu wanasema biashara fulani inalipa, anaingia kwenye biashara hiyo, anaianza na kukutana na changamoto mbalimbali, kabla hajatatua changamoto hizo, anasikia kuna biashara nyingine inalipa zaidi, anaachana na hiyo ya mwanzo na kwenda kufanya mpya.

Mtu anazunguka hivyo kwa miaka mingi, anachoka kweli kweli, lakini akiangalia hakuna mafanikio aliyopata. Siyo kwa sababu hakuweka juhudi, ila kwa sababu hakuweka juhudi hizo kwenye eneo moja kwa muda mrefu.

Hivyo nikukumbushe hili leo rafiki yangu, ili ufanikiwe lazima UJUE KWA HAKIKA NINI UNATAKA, na baada ya kujua hilo, uwe KING’ANG’ANIZI kwa kuweka juhudi kwenye kile unachotaka bila ya kuhangaika na vitu vingine.

Karibu kwenye mazingira yatakayokuwezesha kuvuka kikwazo hicho cha mafanikio.

Rafiki yangu mpendwa, sisi binadamu tuna udhaifu mmoja mkubwa, umakini wetu huwa hautulii eneo moja. Tukiona vitu vipya huwa tunafikiri ni bora kuliko vya zamani.

Na hali hiyo ndiyo imekuwa inapelekea kila wakati tunabadili kile tunachofanya, tukianza kufanya kitu tunakichoka baada ya muda fulani. Na tunaposikia kuna fursa nyingine mpya, hiyo inakamata umakini wetu kuliko fursa tuliyokuwa tunafanyia kazi awali.

Hii ndiyo sababu tumekuwa tunatamanishwa sana na fursa nyingi mpya tunazokutana nazo kwenye maisha. Ni asili yetu, ndivyo tulivyoumba.

Hivyo kama tunataka kufanikiwa, tunapaswa kujiweka kwenye mazingira ambayo yatatulazimisha kufanya kitu kimoja kwa muda mrefu badala ya kuhangaika na vitu vipya kila wakati.

Jamii zetu haziwezi kutusaidia kwenye hili, maana kila mtu anahangaika na vitu vipya na wale unaowaamini ndiyo watakuwa wa kwanza kukuambia unapitwa na vitu vipya.

Kuna mazingira ya tofauti kabisa yatakayokuwezesha kuchagua kile unachotaka na kukifanyia kazi kwa muda mrefu huku ukipuuza mambo mapya yanayokuja kwako kila wakati.

Mazingira hayo ni KISIMA CHA MAARIFA.

Kwa kuwa kwenye KISIMA, unapanga hatua zipi kubwa unazokwenda kupiga kwa miaka kumi ijayo na ni nini utafanya kufikia hatua hizo. Utaeleza ni maeneo yapi unataka kubobea zaidi kwenye maisha yako. Na pia kwenye kila mwaka wa mafanikio, utaeleza lipi lengo lako kuu unalifanyia kazi.

Ukishaahidi mambo hayo, kocha anakuwa anakufuatilia kupitia taarifa za kila mwezi unazokuwa unatuma. Taarifa hizo zinakutaka ueleze hatua ambazo unapiga kwenye yale unayofanyia kazi.

Katika taarifa hizi, kocha akigundua umeanza kuhangaika na mambo mapya na kuacha mpango uliokuwa umeweka, anakukumbusha na kukurudisha kwenye mstari sahihi.

Hili limekuwa na manufaa makubwa kwa wengi, wengi wameacha kuhangaika na vitu vipya vinavyokuja kwao na kuweka juhudi zao kwenye yale machache na juhudi hizo zimeleta matunda makubwa.

Ndani ya KISIMA CHA MAARIFA unazungukwa na watu wengine ambao pia wameshachagua nini wanataka na wanajituma kuhakikisha wanapata kile wanachotaka. Wameshaondoka kwenye zile mbwembwe za kuhangaika na fursa mpya kila wakati na wamechagua kile hasa wanachotaka na kupambana nacho. Hii inafanya KISIMA CHA MAARIFA kuwa jamii sahihi ambapo wote wanaopenda mafanikio makubwa wanapaswa kuwepo.

Rafiki yangu mpendwa, kama bado hujawa mwanachama wa KISIMA CHA MAARIFA, basi jua unajichelewesha sana kufikia mafanikio makubwa. Unajiweka kwenye hatari ya kuendelea kuhangaika na fursa mpya kila wakati na kujichosha huku ukiwa huna matokeo makubwa unayozalisha.

Karibu ujiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo hii, ili upate nafasi ya kuchagua kusudi kuu la maisha yako na ambalo utaliishi na kulifanyia kazi kila siku, huku ukipata uangalizi wa karibu wa kocha ambaye hatakuruhusu uhangaike na mambo yasiyo na manufaa kwako.

Kupata maelezo ya kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA soma maelezo hapo chini.

KARIBU KWENYE KISIMA CHA MAARIFA.

KISIMA CHA MAARIFA ni programu maalumu ya ukocha ambayo naiendesha na inawalenga wale ambao wana kiu ya kutaka kupata mafanikio makubwa kwenye maisha yao. Lakini pia watu hao lazima wawe tayari kujitoa kupata mafanikio hayo, na siyo tu watu wa maneno na mipango mingi bila vitendo.

Kwa kuwa kwenye programu hii ya KISIMA CHA MAARIFA, unanufaika na mambo mengi, machache na kuhimu ni haya;

1. Unakuwa kwenye kundi maalumu la wasap la KISIMA CHA MAARIFA, ambalo ndiyo kundi pekee unaloweza kunipata mitandaoni.

2. Unapata nafasi ya kusoma makala na mafunzo ya semina mbalimbali kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA (www.kisimachamaarifa.co.tz)

3. Unapata nafasi ya kuwa karibu na mimi Kocha wako. Kutokana na majukumu mengi ninayokuwa nayo, nakosa nafasi ya kuweza kuwa karibu na kila anayependa tuwe karibu. Lakini muda mchache ninaoupata, nauweka kwenye KISIMA CHA MAARIFA. Hivyo kama unataka tuwe karibu, upate ushauri wowote kutoka kwangu moja kwa moja basi unapaswa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA.

4. Kila siku unaianza siku yako kwa TAFAKARI nzuri inayokufikirisha na kukuhamasisha kwenda kufanya makubwa kwenye siku yako. Tafakari hizi zinapatika kwenye kundi la wasap la KISIMA CHA MAARIFA pekee.

5. Unapata nafasi ya kushiriki mijadala mbalimbali ya mafanikio kwa kushirikiana na wengine walio kwenye safari hiyo ya mafanikio kwenye kundi la wasap.

6. Kila mwezi unapata nafasi ya kuitathmini kuona ni hatua zipi unazopiga kufikia lengo ulilojiwekea. Na tathmini hiyo unanitumia mimi Kocha wako, ambapo naipitia na kukushauri pale penye uhitaji huo.

7. Kwa kuwa kwenye KISIMA CHA MAARIFA unapata nafasi ya kukutana ana kwa ana na watu wenye mtazamo wa mafanikio na wanaopambana kufanikiwa kama wewe. Kuna KLABU ZA KISIMA CHA MAARIFA ambazo zinawaleta pamoja wanachama walio mkoa au wilaya moja.

8. Unapata nafasi ya kupata huduma nyingine za ukocha ninazotoa, kama ukocha wa mtu mmoja mmoja (PERSONAL COACHING) na ukocha wa vikundi kama GAME CHANGERS na LEVEL UP.

9. Kila siku unapata makala ya UKURASA WA MAISHA YA MAFANIKIO, hizi ni makala zinazowekwa kila siku kwenye tovuti ya KISIMA CHA MAARIFA. Makala hizi ni fupi na zimebeba ujumbe muhimu ambao unakujengea uwezo wa kufanya maamuzi bora kwa kila hali unayopitia kwenye maisha yako.

10. Kila mwaka huwa kuna mkutano wa pamoja wa wanachama wote wa KISIMA CHA MAARIFA, hapo unapata nafasi ya kukutana na wengine, kujifunza kupitia hatua wanazopiga na hata kujenga mtandao wako wa mafanikio.

Rafiki, kwa manufaa hayo kumi niliyokushirikisha na mengine mengi, tukisafiri pamoja, hutaweza kubaki pale ulipo sasa.

Ili kupata manufaa hayo na mengine mengi, unapaswa kujiunga na KISIMA CHA MAARIFA. Na kujiunga unalipa ada ya mwaka ambayo kwa sasa ni tsh 100,000/= (laki moja). Huo ni uwekezaji ambao utaufanya na utakulipa sana, kwani manufaa utakayoyapata, ni zaidi ya mara 10 ya ada hiyo.

Karibu ujiunge sasa kwa kutuma ada yako kwenda namba 0717396253 na ukishatuma ada, tuma ujumbe kwa njia ya wasap kwenda namba hiyo 0717396253 wenye majina yako na maelezo kwamba umelipia KISIMA CHA MAARIFA na utaunganishwa ili tuweze kusafiri pamoja.

Hii siyo fursa ya kuikosa rafiki yangu, huna kinachokuzuia bali wewe mwenyewe, chukua hatua sasa na kwa pamoja tukafanye makubwa kwenye muongo huu wa 2020 – 2030.

Jiunge na KISIMA CHA MAARIFA leo kwa kulipa ada tsh 100,000/= kwa namba 0717396253 na utapata nafasi ya kuingia kwenye jamii hii ya tofauti kabisa itakayokuwezesha kupiga hatua kubwa kwenye maisha yako.

Rafiki, kama ungependa kuendelea kupokea makala na mafunzo mengine mazuri kwenye email yako, fungua hapa na ujaze fomu; www.bit.ly/amkaemail  

Makala Hii Imeandikwa Na Dr. Makirita Amani Ambaye Ni Daktari Wa Binadamu, Kocha Wa Mafanikio, Mwandishi Na Mjasiriamali.

Kupata vitabu na uchambuzi wa kina wa vitabu jiunge na channel ya SOMA VITABU TANZANIA kwa kufungua kiungo hiki; www.t.me/somavitabutanzania