“Whenever you ask whether you should behave in this way or the other, ask yourself, what would you do if you knew that you could die this evening, and nobody would find out about your action? Death spurs people to finish their affairs; among all actions, there is only one type which is complete, and that is love which seeks no reward.” – Leo Tolstoy
Pale unapojikuta njia panda,
Ukiwa upo kwenye mambo yanayokinzana na hujui ufanye lipi,
Ni rahisi kupoteza muda wa kuendelea na mvutano ulio ndani yako na kutokufanya chochote.
Lakini mvutano huo hauna manufaa yoyote kwako kama hakuna hatua unayochukua.
Na kwa kila hali unayokuwa unapitia, kuna kilicho sahihi kufanya,
Ila mara nyingi kilicho sahihi kufanya, siyo kinachotuvutia kufanya.
Na hilo ndiyo linalotuweka njia panda,
Ufanye kilicho sahihi lakini hukipendi au ufanye unachopenda lakini siyo sahihi?
Njia pekee ya kuvunja hali hiyo ya ukinzani na kufanya maamuzi ya kipi ufanye,
Ni kutumia kifo.
Jiulize kama leo itakuwa siku yako ya mwisho hapa duniani, ungefanya nini?
Ni rahisi kuahirisha mambo na kuendelea na mvutano ndani yako pale unapojua kesho ipo.
Lakini kesho inapofutika na ukabaki na leo tu, ghafla mtazamo unabadilika.
Unaona kile tu kilicho sahihi kufanya na siyo vitu vingine.
Utambuzi wa kifo unasukuma watu kukamilisha yale yaliyo sahihi na muhimu.
Utumie kila unapojikuta njia panda na maanisha kweli.
Kwa sababu ipo siku hilo litatimia, kwa kuwa hujui siku hiyo ni lini, basi chukulia ni kila siku.
#NidhamuUadilifuKujituma
#AfyaUtajiriHekima
#KaziUpendoHuduma
Wako rafiki katika safari ya kuelekea kwenye mafanikio makubwa,
Kocha Dr Makirita Amani,
http://www.t.me/somavitabutanzania